Dini nchini Burkina Faso
Mandhari
Dini nchini Burkina Faso zinachanganyikana kwa sababu mtu yuleyule anaweza kuwa Mwislamu au Mkristo pamoja na kufuata mambo ya mila.
Serikali ya Burkina Faso ilikadiria katika sensa ya 1996 kuwa asilimia 60 ya watu ni Waislamu, wengi wao wakiwa Sunni, pamoja na wachache wa Shia na Sufi wa Tijaniyah au Salafi.[1] Pia kuna wafuasi wa Uislamu wa Ahmadiyya. Takriban asilimia 24 hufuata dini za jadi za Kiafrika, asilimia 17 ni Wakatoliki, na asilimia 3 ni Waprotestanti.[1]
Kufikia mwaka 2019 ilikadiriwa Waislamu kuwa 63.8%, Wakristo kuwa 26.3% (Wakatoliki 20.1 na Waprotestanti 6.2%), huku wafuasi wa dini za jadi wamepungua hadi kuwa 9% tu.
Miaka ya mwisho Wakristo wengi wameuawa na Waislamu, hivi kwamba ni hatari kwao kuishi nchini [2]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |