Nenda kwa yaliyomo

Diane Kruger

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Diane Kruger

Amezaliwa Diane Heidkrüger
15 Julai 1976 (1976-07-15) (umri 48)
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi 2002–mpaka sasa
Ndoa Guillaume Canet (m. 2001–2006) (ametalikiwa)

Diane Kruger (alizaliwa kama Diane Heidkrüger mjini Algermissen, karibu na Hildesheim, Ujerumani, 15 Julai 1976) ni mwigizaji wa filamu na mwanamitindo wa zamani kutoka nchini Ujerumani.

Huko Amerika ya Kaskazini, anafahamika zaidi kwa uhusika wake wa Helen kwenye filamu ya Troy, Dr. Abigail Chase kwenye National Treasure na National Treasure: Book of Secrets, na Bridget von Hammersmark kwenye Inglourious Basterds.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Kruger ni binti wa mwajiriwa wa benki Maria-Theresa na mtaalamu wa masuala ya kompyuta Bwana Hans-Heinrich Heidkrüger.[1] Alilelewa katika mazingira ya Kanisa Katoliki[2] kuhitimu elimu yake ya awali katika shule za Kikatoliki.

Diane hakuwahi kunywa pombe hadi alipofikisha umri wa miaka 20, kwa sababu aliona kasoro na athari za ulevi kupitia kwa baba yake.[3] Mama yake alimsomesha Diana katika vipindi tofauti ili aongeze tija lugha ya Kiingereza kwa mwanawe. Alilelewa nchini Ujerumani akiwa na mdogo wake wa kiume, Stefan.

Akiwa msichana, Kruger alitaka hasa kuwa ballerina na kwa bahati akafanikiwa kuchaguliwa kwenye shule ya balleti ya Royal Ballet School ya mjini London. Hata hivyo, baada ya kuumia imepelekea aache kazi ya ballet ikiwa bado changa kabisa, Kruger akahamia mjini Paris na kubadilisha nguvu zake upande wa uanamitindo.[4]

Diane Kruger, Cannes Film Festival 2009
  1. "Diane Kruger Biography". Filmreference.com. Iliwekwa mnamo 2010-05-30.
  2. "Diane Kruger for Marie Claire". Marie Claire. 2010-04-01. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-05-02. Iliwekwa mnamo 2010-07-15. This month, she speaks openly to Marie Claire about a difficult childhood, her Catholic upbringing...
  3. Friedlander, Noam. "Diane Kruger interview", The Telegraph, 2009-06-02. Retrieved on 25 Januari 2010. 
  4. "AskMen.com". AskMen.com. 1976-07-15. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-10-04. Iliwekwa mnamo 2010-05-30.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: