Dhow Countries Music Academy
Dhow Countries Music Academy (DCMA) ni shule ya muziki ya kwanza na ya pekee huko Zanzibar, Tanzania, iliyopo katika Nyumba ya Culture Club barabara ya Vuga Road•
Chuo hicho kinasaidia na kuhifadhi urithi wa muziki wa "taarabu" unaojumuisha nchi zilizopo kando ya mwambao wa Bahari ya Hindi na Ghuba ya Uajemi. Madhumuni maalum ni kufundisha muziki wa jadi, kama vile Taarab, Kidumbaki na Ngoma.
"Katika miaka ya hivi karibuni, Chuo hiki cha Muziki cha Kisiwa cha Tanzania kimekuwa kituo muhimu cha mkutano wa eneo la utamaduni wa ndani."[1]
Madhumuni
[hariri | hariri chanzo]Chuo hichi kilianzishwa mnamo mwaka 2002 na kwa miaka mingi kilikuwa na wanafunzi zaidi ya 1500. DCMA ni mmoja ya wajumbe maarufu wa muziki wa taarab ulimwenguni. Kimepata sifa inayoongezeka kimataifa ya kufundisha muziki wa jadi. Mnamo mwaka 2007, Hildegard Kiel, mkurugenzi na mwanzilishi wa DCMA alichaguliwa kwenye tuzo ya BBC World Music Award, wakitambua mchango wake mkubwa katika kufufua urithi wa muziki wa Zanzibar na anga ya muziki ulimwenguni kote. Mnamo Oktoba 2010 DCMA ilishinda Tuzo ya Muziki ya Roskilde kwa kufundisha muziki wa jadi.[2]
Katika mafunzo ya wanafunzi nikuhakikisha na kuendeleza Ujuzi na maarifa ya urithi wa kipekee wa muziki wa kitamaduni. Chuo cha Muziki cha Dhow Countries Music Academy kilichukua jina lake kutoka katika meli ya kitamaduni, jahazi, iliyoundwa na Waarabu, nakutumika katika eneo la Bahari ya Hindi. Rasi ya Arabia ina historia tajiri ya usafiri wa bahari na kubadilishana utamaduni na pwani ya Afrika Mashariki. Jahazi zimetumika katika eneo hili kwa karne nyingi, na zilikuwa muhimu katika kukuza uvuvi, kuzamia lulu na biashara pamoja na mabadilishano ya kitamaduni. DCMA ni kituo kikuu cha mafundisho na utendaji wa utamaduni wa muziki ambao walisafiri kwa meli kutoka Mashariki ya Kati hadi Afrika kupitia Bahari ya Hindi.
Dhamira ya Chuo cha Muziki cha Dhow Countries Music Academy ni kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha tasnia ya muziki wa Zanzibar kwa kufanya utafiti, kuhifadhi, kutoa mafunzo, kukuza na kuendeleza urithi wa muziki wa Zanzibar na "Dhow Countries", zote kikanda na kimataifa. Kabla ya DCMA kuanzishwa, muziki wa asili Zanzibar ulikuwa karibu kusahaulika. Kulikuwa na vikundi kadhaa vya asili ya taarab, na ni vijana wachache sana waliokuwa tayari kutunza urithi huo. Lakini tangu DCMA ianzishe dhamira yake hali ilibadilika, muziki wa kitamaduni na Wanamuziki wakitamaduni walizidi kuongezeka.
Elimu ya muziki
[hariri | hariri chanzo]Mtaala wa DCMA unatoa elimu bora kuanzia mwanzo hadi ngazi ya juu. Kozi za cheti na diploma ni pamoja na kozi za nadharia ya muziki wa Waswahili hasa watu wa Zanzibar, yaani muziki wa Mashariki-Kiarabu. Ingawa ni maalumu katika muziki wa jadi wa Kiarabu na Kiafrika katika eneo hilo, DCMA pia hutoa fursa kwa wanafunzi kujifunza zana zinazotumika katika utamaduni wa muziki wa Magharibi. Mafunzo ya muziki katika DCMA yanajumuisha:
- Mafunzo ya chombo na sauti kupitia masomo ya kibinafsi na ya darasa. Masomo haya yanazingatia ujuzi wa utendakazi kwenye vyombo mbalimbali ikijumuisha Fidla, oud, zeze, gitaa, piano, kinanda cha kielektroniki, Kiarabu, Kinanda cha Mkononi na filimbi.
- Mafunzo ya kiwango cha cheti na diploma katika masomo ya utendaji ambayo pia yanajumuisha kozi ya muziki wa kitamaduni wa Kiarabu na Kiafrika na njia za kutafiti utamaduni huo.
Wakati lengo kuu la DCMA ni kuhifadhi na kukuza urithi wa muziki wa Zanzibar, katika miaka ya hivi karibuni imeanzisha kozi za muziki katika utamaduni na masomo maalum, matamasha na eneo la kazi na wahandisi wa sauti, washirika wa tamasha kutoka kote ulimwenguni na wanamuziki wa kitaaluma, kama Cleveland Watkiss, Oliver Mtukudzi, Ricardo Garcia, Blitz the Ambassador, Moussa Diallo, Harald Lassen, Florian Ross, Grzegorz Niemczuk, Leon Michael King, Piotr Damasiewicz, Derek Gripper, Makadem na wengine.
Zaidi ya hayo, DCMA hutoa semina maalum, ziara za kubadilishana na shughuli za mtandao mwaka mzima, kwa mfano, mkutano wa Kumbukumbu, Nguvu na ujuzi katika Muziki wa Kiafrika na Zaidi, mnamo Juni 2015, iliwasilishwa kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu vya Ghana na Nigeria katika Afrika Magharibi na Chuo cha Johannes Mainz na Chuo cha Hildesheim nchini Ujerumani.[3]
Elimu kwa watoto
[hariri | hariri chanzo]DCMA inatoa masomo ya muziki ya bure kwa zaidi ya watoto 100 katika shule 6 za msingi huko Zanzibar. Kujifunza muziki kuna faida nyingi kwa watoto. Inasaidia ukuaji wao wa kielimu, kijamii na kihisia. Huendeleza ujuzi wa lugha. Utafiti umeonyesha kuwa wale wanaofanya elimu ya muziki wana matokeo bora katika mitihani kwa kiwango cha juu kuliko kawaida. Pia wanapata alama za juu katika shule ya sekondari. Elimu ya muziki huendeleza ujuzi ambao ni muhimu katika mahali pa kazi. DCMA pia inasaidia watoto wenye ulemavu mbalimbali. Tangu mwaka 2012 DCMA imefundisha katika Shule ya Msingi Kisiwadui kikundi cha watoto wenye ulemavu wa viungo yaani upofu, matatizo ya kusikia na wanaotembelea viti vya magurudumu. Mwaka huu Chuo kilianza kufanya kazi na shirika la NGO ndani ya Kahesa Zanzibar na inatoa elimu ya muziki bila malipo kwa watoto wenye ugonjwa wa vinasaba na usonji.
Shughuli za elimu ya uenezi
[hariri | hariri chanzo]Pamoja na shughuli zake katika Mji Mkongwe, Zanzibar, DCMA ilianza mpango wa kufikia watu wa vijijini ili kujibu maombi ya jumuiya za vijijini kuleta elimu ya muziki na ujuzi wa uimbaji wa muziki katika maeneo ya mbali zaidi. Hii ni kweli hasa kwa maeneo yale ambapo vikundi vidogo vya ala za kitamaduni vinaendelea kuwepo na kuhangaika kuishi. Mahonda, kijiji kidogo karibu kilomita 25 nje ya Mji Mkongwe, ni mwanachama wa Chuo hichi cha Muziki. Kazi za DCMA katika Mahonda zinalenga watu ambao tayari wana ujuzi fulani katika muziki, kuwawezesha kusambaza ujuzi wao kwa wengine mara kwa mara. Wanafunzi waliofanikiwa wamealikwa kusoma muda wote huko DCMA katika Mji Mkongwe, ambayo inawaongoza kwenye ngazi ya vyeti na ngazi ya diploma.
Bendi za DCMA
[hariri | hariri chanzo]Bendi za DCMA, wanafunzi na walimu hutembelea Zanzibar mara kwa mara ili kuimarisha maisha ya kitamaduni ya Zanzibar kupitia matamasha na maonyesho katika vilabu na migahawa. kwa mfano, matamasha ya Taarab na muziki wa Afro, hivyo hushirikisha muziki wa Afro-fusion, jazz, afrobeat na bongo-flava. Zaidi ya hayo, DCMA huandaa mara kwa mara michuano maalum ya wanamuziki wa kimataifa na warsha za umma za Ngoma. Baadhi ya bendi zilizotoka DCMA zimepata heshima za kimataifa nje ya Zanzibar:
- Taarab / Kidumbak Ensemble inawakilisha muziki wa kitamaduni wa magharibi mwa Bahari ya Hindi, mitindo ya ala na sauti ya mchanganyiko huu wa muziki wa Kiarabu na Kiafrika.[4]
- Mapanya Band, iliyoanzishwa mwaka wa 2016, ni moja ya makundi ya vijana yenye matumaini zaidi huko Zanzibar na inamchanganyiko wa kipekee wa Afro-Fusion, Hip-Hop na Reggae.[5]
- Siti and the Band, ilianzishwa mwaka wa 2015, kama waimbaji na wachezaji wa oud Siti Amina, Rahma Ameir (zeze) na Gora Mohammed (Qanun) waliamua kujitolea kwenye muziki wa Taarab kwa ushawishi wao binafsi ili kuunganisha muziki.[6]
- Mcharuko inawakilisha Zanzibar na Dar es Salaam tangu mwaka 2017, pamoja na mchanganyiko wa mitindo maarufu ya muziki ya Kiafrika iliyoongozwa na Christopher Anthony (filimbi ya jazz), yenye gitaa, ngoma na sauti.
- Afro Jazz Group, mchanganyiko wenye nguvu wa mitindo ya Kiafrika, Kiarabu na mtindo wa Magharibi.
- Vilevile DCMA Ngoma Group, inayoongozwa na nguli wa ngoma Zanzibar Mzee Kheri.
Maonyesho ya kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Tangu DCMA ianzishwe, vikundi vingi vimejitokeza kwenye matamasha nchini Tanzania, nchi nyingine za Afrika na sehemu nyingine za duniani, kwa mfano, kila mwaka vikundi vya DCMA vinashiriki katika Tamasha la Sauti za Busara huko Zanzibar; mwaka 2005 kikundi cha taarab cha DCMA kilishiriki katika Tamasha la Mela nchini Ufaransa, mwaka 2015 kundi la taarab la DCMA lilishiriki katika Tamasha la Shujaa huko Wroclaw, Poland, katika tamasha la Afrika huko Würzburg, Ujerumani, mwaka 2016 kwenye Tamasha la Orient Tallinn, Estonia ilisema machache tu katika maonyesho hayo ya kimataifa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Luca Beti: Sansibars bewegende Rhythmen. In: One World. 02/2018, p. 38-40, full text
- ↑ World Music Award 2010 of Roskilde Festivals for DCMA
- ↑ "University of Hildesheim: Center for World Music Congress, DCMA, June 2015". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-27. Iliwekwa mnamo 2022-02-18.
- ↑ „Music in Africa“ Portal about taarab-kidumbak-Ensemble
- ↑ „Music in Africa“ Portal about Mapanya-Band
- ↑ „Music in Africa“ Portal about Siti-and-the-Band