Nenda kwa yaliyomo

Devolent Mtui

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dkt. Devolent Mtui ni mwanasayansi na mtafiti wa wanyamapori kutoka nchini Tanzania. Anajulikana sana kwa ugunduzi wake wa spishi mpya ya kipepeo iitwayo Charaxes mtuiae katika bonde la Kihansi, nchini Tanzania.[1]

Elimu na Kazi

[hariri | hariri chanzo]

Dkt. Mtui anafanya kazi kama mtafiti katika Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), iliyo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.[1]

Mnamo mwaka 2017, akiwa kwenye utafiti wa nyanjani katika misitu ya Bonde la Kihansi, alikusanya na kuchunguza takriban spishi 200 za vipepeo, jambo lililopelekea kugunduliwa kwa spishi mpya ya kipepeo ambayo haikuwahi kuwekwa kwenye kumbukumbu za kisayansi duniani.[1][2]

Spishi hiyo mpya ilipewa jina la kisayansi la Charaxes mtuiae kwa heshima ya jina lake. Vipepeo huchukuliwa kama viashiria muhimu vya ekolojia, na ugunduzi huo uliongeza uelewa wa tofauti za kibiolojia ika mazingira ya kipekee ya ikolojia ya Tanzania.[1]

  1. 1 2 3 4 "Tanzanian Scientist Dr. Devolent Mtui Expands Global Biodiversity with Discovery of New Butterfly Species". Tanzania Wildlife Research Institute (TAWIRI). 5 Machi 2026. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2026-09-16. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2026.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. ↑ "Mwanasayansi wa Tanzania agundua spishi mpya ya kipepeo". BBC Swahili. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2026.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Devolent Mtui kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.