Desperate Housewives

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Desperate Hoisewives

Nembo ya Desperate Housewives
Aina Vichekesho
Imetungwa na Marc Cherry
Nchi inayotoka Marekani
Lugha Kiingereza
Ina misimu 7
Utayarishaji
Watayarishaji
wakuu
Marc Cherry
Tom Spezialy (seasons 1-2)
Michael Edelstein (seasons 1-2)
Joe Keenan (season 3)
George W. Perkins (seasons 3-4)
Bob Daily (season 4)
John Pardee & Joey Murphy (season 4)
Kevin Murphy (co-exec)
Chris Black (co-exec, season 2)
Larry Shaw (co-exec, season 3)
David Grossman (co-exec, season 3)
Muda makisio ni dk. 43
Urushaji wa matangazo
Kituo ABC
Viungo vya nje

Desperate Housewives ni kipindi cha Marekani kilichotungwa na Marc Cherry na kutayarishwa na ABC Studios pamoja na Marc CHerry Productions. Watayarishaji wakuu tangu msimu wa nne ni Marc Cherry, Bob Daily, George W. Perkins, John Pardee, Joey Murphy, David Grossman, Larry Shaw na Sabrina Wind.

Kipindi hiki kinawashirikishwa waigizaji wafuatao: Teri Hatcher kama Susan Mayer, Felicity Huffman kama Lynette Scavo, Marcia Cross kama Bree Van de Kamp na Eva Longoria Parker kama Gabrielle Solis. Brenda Strong ndiye muelezaji hadithi.

Tangu ilipoanza kwenye stesheni ya ABC mnamo 3 Oktoba 2004, kipindi hiki kimepata sifa nzuri kuotka watazamaji. Imeshinda tuzo zza Emmy Award na Golden Globe Award na tangu Aprili 2007, iliripotiwa kuwa kipindi kilicho maarufu zaidi kulingana na namba ya watazamaji kote duniani, ikiwa na watazamaji takriban milioni 120.[1]

Misimu[hariri | hariri chanzo]

Msimu wa kwanza[hariri | hariri chanzo]

Desperate Housewives ilianza kuonyeshwa mnamo 3 Oktoba 2004 na inahusu watu wanne wakuu: Susan Mayer, Lynette Scavo, Bree Van de Kamp na Gabrielle Solis, pamoja na familia zao na majirani walioko kwenye barabara ya Wisteria Lane. Mada kuu ya msimu huu ni kujiua kwa Mary Alice Young. Bree anapigania kuokoa ndoa yake, Lynette anajitahidi kulea watoto wake watukutu, Susan anashindana na Edie ili kupata mapenzi ya Mike, na Gabrielle anajaribu kuficha uhusiano wake wa kando na John. Msimu huu unaisha pindi watu wote wanaamini kuwa Bree amempa sumu na kumuua mumewe, Carlos kujulushwa kuhusu uhusiano wa kando wa Gaby kabla ya yeye (Carlos) kupelekwa jela.

Msimu wa pili[hariri | hariri chanzo]

Ilianza mnamo 25 Septemba 2005 na mada yake kuu ni kuhusu jirani mpya aliyehamia Wisteria Lane saa sita za usiku. Katika msimu huu, Bree anajitahidi na maisha ya kuwa mjane, na hatimaye anaanza kulewa. Mtalaka wa Susan anapendana na Edie, na Lynette anapata kazi nzuri na kuwa meneja wa mumewe na Gabrielle anawacha mipango yake ya kando na ana azma ya kuwa na mimba ili kuanza familia. Inapoisha, Mike anagongwa na gari na Orson - ambaye atakuwa mumewe Bree kwenye msimu ujao.

Msimu wa tatu[hariri | hariri chanzo]

Ilianza 24 Septemba 2006. Bree anaolewa na Orson. Vilevile, Lynette anajitahidi kukabiliana na mwana wa kando wa mumewe. Tom anafungua mkahawa unaozidisha mzozo kati yake na mkewe. Gabrielle anawachana na mumewe na kupendana na Meya wa Fairview. Edie bado anamshawishi Mike kimapenzi. Susan naye anapendana na Muingereza mmoja aliye na mkewe mgonjwa mahututi.

Msimu wa nne[hariri | hariri chanzo]

Ilianza 30 Septemba 1997,[2] na mada yake kuu ni kuhusu Katherine Mayfair na familia yake. Hata hivyo, Lynette anakabiliana na saratani; Gabrielle, aliyeolewa na Meya, anaanza mpango wa kando na mtalaka wake Carlos; Susan na Mike wanafurahia maisha yao kama maharusi. Mashoga wawili wanaguria Wisteria Lane - Lee na Bob. Upepo mkali unakuja na kuvunja nyumba zote kwenye barabara ya Wisteria Lane.

Msimu wa tano[hariri | hariri chanzo]

Ilianza mnamo 28 Septemba 2008. Mada kuu ni kuhusu mumewe Edie Britt anayeitwa Dave Williams. Dave anataka kulipiza kisasi kwa mtu anayeishi Wisteria Lane. Lynette na Tom wanagundua kuwa mwana wao anapendana na mwanamke aliyeolewa. Carlos na Gabrielle wanakabiliana na watoto wawili: Juanita na Celia. Bree na Orson wanapata tabu kwenye ndoa yao. Orson anaanza tabia ya kuiba kutoka kwa majirani.

Msimu wa sita[hariri | hariri chanzo]

Ilianza Jumapili, 27 Septemba 2009 saa tatu jioni.[3] Mada kuu ni kuhusu mpango wa kando wa bree na Karl. Vipindi vilivyobaki 13 vitaendelea mnamo 3 Januari 2010.

Wahusika Wakuu[hariri | hariri chanzo]

 • Teri Hatcher aliigiza kama Susan Mayer, mama aliyetalikiwa na angali akitafuta mpenzi.
 • Felicity Huffman aliigiza kama Lynette Scavo, mama wa watoto wanne.
 • Marcia Cross aliigiza kama Bree Van de Kamp
 • Eva Longoria Parker aliigiza kama Gabrielle Solis, ambaye ni mwanamitindo na aliyeanza mpango wa kando na kijana wa miaka 17.
 • Nicollette Sheridan aliigiza kama Edie Britt, adui wa Susan.
 • Ricardo Antonio Chavira aliigiza kama mumewe Gabrielle, aitwaye Carlos Solis.
 • James Denton aliigiza kama Mike Delfino, mpenzi wa Susan.
 • Doug Savant aliigiza kama Tom Scavo, mumewe Lynette.

Mafanikio[hariri | hariri chanzo]

Msimu Saa Mwanzo wa msimu Mwisho wa msimu Msimu wote Namba Watazamaji (milioni)
1 Sunday 9:00 P.M. 4 Oktoba 2004 22 Mei 2005 2004-2005 #4[4] 23.8[4]
2 Sunday 9:00 P.M. 25 Septemba 2005 21 Mei 2006 2005-2006 #4[5] 21.7[5]
3 Sunday 9:00 P.M. 24 Septemba 2006 20 Mei 2007 2006-2007 #10[6] 17.5[6]
4 Sunday 9:00 P.M. 30 Septemba 2007 18 Mei 2008 2007-2008 #6[7] 18.6[7]
5 Sunday 9:00 P.M. 28 Septemba 2008 17 Mei 2009 2008-2009 #9[8] 15.6[8]
6 Sunday 9:00 P.M. 27 Septemba 2009 Mei 2010 2009-2010 #20 14.9

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Dana Delany, Teri Hatcher, Brenda Strong na Andrea Bowen kwenye tuzo za GLAAD Media Awards
 • Mnamo 2006, kipindi hiki kilipata tuzo ya Golden Globe for Best TV Musical or Comedy Series.
 • Mnamo 2005, ilishinda tuzo la People's Choice Award for Favorite New Television Drama.[9]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Desperate Housewives On SABC3 Confirmed, TVSA News Desk, 3 Aprili 2007
 2. ABC Announces Fall Première Dates, The Futon Critic, 25 Julai 2007
 3. "ABC Announces Fall Premiere Dates for 19 Shows". TVGuide.com. Iliwekwa mnamo 2009-06-09.
 4. 4.0 4.1 "Season Program Rankings from 09/20/04 through 05/22/05". ABC Medianet. 24 Mei 2005. Iliwekwa mnamo 2009-07-03.
 5. 5.0 5.1 "Season Program Rankings from 09/19/05 through 05/28/06". ABC Medianet. 28 Mei 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-10-11. Iliwekwa mnamo 2009-07-03.
 6. 6.0 6.1 "Season Program Rankings from 09/18/06 through 06/03/07". ABC Medianet. 3 Juni 2007. Iliwekwa mnamo 2009-07-03.
 7. 7.0 7.1 "Season Program Rankings from 09/24/07 through 05/25/08". ABC Medianet. 28 Mei 2008. Iliwekwa mnamo 2009-07-03.
 8. 8.0 8.1 "Season Program Rankings from 09/22/08 through 05/17/09". ABC Medianet. 19 Mei 2009. Iliwekwa mnamo 2009-07-03.
 9. The IMDb.com list of awards for Desperate Housewives, Retrieved 3 Agosti 2007