Nenda kwa yaliyomo

Dennis Prager

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dennis Prager (2 Agosti 1948) ni mtangazaji wa redio na mwandishi kutoka Marekani. Anajulikana kwa kipindi chake cha kitaifa cha The Dennis Prager Show na kwa kuanzisha PragerU mwaka 2009.PragerU ni shirika lisilo la faida aliloanzisha akishirikiana na Allen Estrin kwakutengeneza video fupi mtandaoni zenye maudhui ya kielimu kuhusu historia, siasa, uchumi, dini, na utamaduni.

Prager alizaliwa Brooklyn katika familia ya Kiyahudi. Alisomea anthropolojia na historia katika Chuo cha Brooklyn (B.A. 1970), na baadaye aliendelea na masomo huko Columbia na Leeds.

Mnamo 1975, alishirikiana na Joseph Telushkin kuandika kitabu cha The Nine Questions People Ask About Judaism, kitabu kilichouzwa sana kikielezea Uyahudi kwa hadhira ya wasiofuata dini. Kuanzia 1976 hadi 1983, aliendesha Taasisi ya Brandeis-Bardin. Baadaye, kupitia maandiko na vipindi vyake, alijulikana kwa ukosoaji wake wa maadili ya kidunia na tabia ya ubinafsi, akihimiza maadili ya kitamaduni na dini kama msingi wa jamii yenye mshikamano.[1][2][3]

  1. ↑ "Kallah participants to hear Dennis Prager". The Jewish Press [Omaha, Neb]. Desemba 11, 1981.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. ↑ Friedman, Murray (2003). "The Changing Jewish Political Profile". American Jewish History. 91 (3/4): 423–438. doi:10.1353/ajh.2005.0008. JSTOR 23887289. S2CID 153461672.
  3. ↑ Kirsch, Jonathan (Mei 16, 2018). "A Rational View of the Torah". Jewish Journal. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Desemba 21, 2018. Iliwekwa mnamo 13 Julai 2018.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dennis Prager kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.