Hongo (nyoka)
(Elekezwa kutoka Dendroaspis)
Jump to navigation
Jump to search
Hongo | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Hongo mashariki
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 4:
|
Hongo, futa au koboko ni nyoka wenye sumu wa jenasi Dendroaspis katika nusufamilia Elapinae (familia Elapidae). Spishi zote zinatokea Afrika tu. Nyoka hawa huishi mitini, lakini futa hukaa chini. Huwinda wakati wa mchana na kukamata mamalia wadogo, ndege na mijusi. Hawa ni hatari sana kwa sababu sumu yao ni kali sana. Kuna liga za neva na za moyo ndani yake. Sumu ya futa ni kali zaidi kuliko ile ya spishi nyingine. Kwa hivyo nyoka huyu ni mgomvi zaidi. Sumu yake inaweza kuua mtu mzima ndani ya nusu saa.
Spishi[hariri | hariri chanzo]
- Dendroaspis angusticeps, Hongo Mashariki au Koboko Kijani (Eastern green mamba)
- Dendroaspis jamesoni, Hongo wa Jameson (Jameson's mamba)
- Dendroaspis polylepis, Hongo Mweusi, Futa au Koboko (Black mamba)
- Dendroaspis viridis, Hongo Magharibi (Western green mamba)
Picha[hariri | hariri chanzo]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.