Demografia ya Kenya
Demografia ya Kenya | |
---|---|
![]() |
|
Idadi ya watu | |
Idadi ya watu (2024) | ▲ 52,428,290 [1] |
Msongamano | 99/km² |
Mijini | 31% [1] |
Vijijini | 69% [1] |
Ukuaji na Mabadiliko | |
Kiwango cha Ukuaji | ![]() |
Kiwango cha kuzaliwa | ![]() |
Kiwango cha kufa | 6.2 kwa kila 1,000 |
Umri wa Kuishi | ▲ 63.8 miaka |
Kiwango cha uzazi | ![]() |
Muundo wa Umri | |
Umri wa wastani | ▲ 19.8 (2024) [1] |
0-14 | 37.2% [3] |
15-24 | 20.45% [3] |
25-54 | 33.5% [3] |
55-64 | 4.01% |
65+ [3] | 3.1% |
Lugha | |
Lugha Rasmi | Kiswahili, Kiingereza |
Demografia ya Kenya inafuatiliwa na Ofisi ya kitaifa ya takwimu ya Kenya (KNBS). Sensa ya mwisho kufanyika ilikuwa mwaka wa 2019, sensa za awali zilikuwa na utata. Kulingana na KNBS Kenya ina watu milioni 52 mnamo 2024. [4] [5]
Idadi ya Watu
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 2024, Kenya inakadiriwa kuwa na wakazi milioni 54.7. Kulingana na Sensa ya Kitaifa ya 2019, jumla ya idadi ya watu ilikuwa 47,564,296. Kiwango cha ukuaji wa idadi ya watu kinazidi kupunguka kutoka 4.1% mwaka 1966, 2.9% mwaka 2010 hadi 1.9% mwaka 2024. Umri wa wastani wa wakazi wa Kenya ni miaka 19.4.
Ukuaji wa Idadi ya Watu kwa Miaka
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Idadi ya Watu |
---|---|
1948 | Milioni 5.4 |
1962 | Milioni 8.3 |
1969 | Milioni 10.9 |
2000 | Milioni 31.4 |
2025 | Milioni 53 |
Kabila na Asili
[hariri | hariri chanzo]Kenya ina zaidi ya makabila 40, yanayojumuishwa katika Wabantu, Waniloti, Wakushi, na jamii nyingine ndogo. Makabila makubwa zaidi ni:
- Wakikuyu – 17.1%
- Waluhya – 14.3%
- Wakalenjin – 13.4%
- Wajaluo – 10.7%
- Wakamba – 9.8%
- Wasomali – 5.8%
- Wakisii – 5.7%
- Wamijikenda – 5.2%
- Wameru – 4.2%
- Makabila mengine – 13.8%
Lugha
[hariri | hariri chanzo]Kenya ina lugha rasmi mbili, Kiswahili na Kiingereza, ambazo zinatumika kote nchini. Zaidi ya lugha 60 za asili huzungumzwa na makabila mbalimbali.
- Kiswahili: Ni lugha ya taifa na inazungumzwa na watu wengi kama lugha ya kwanza au ya pili.
- Kiingereza: Hutumika katika serikali, biashara, na elimu.Kenya huzungumza Kiingereza cha Britania.
Lugha za Kenya huwa kwa mgawanyiko miwili za Niger Congo na Nilo-Sahara.
Mifano
[hariri | hariri chanzo]- Bantu
- Kikuyu 8.1 milioni
- Kikamba 4.7 milioni
- Kiluhya 1.0 milioni(pamoja na Kibukusu 1.2 milioni)
- Kigusii 2.7 milioni
- Kimeru 2.0 milioni
- Kimijikenda/Kigiriama 1 milioni
- Nilotiki
- Kidholuo 5.0 milioni
- Kikalenjin 4.6 milioni (Kipsigis 1.9 milioni, Kinandi 940,000)
- Kimaasai 1.2 milioni (1.9 milioni pamoja na Tanzania)
- Kiturkana 1.0 milioni
- Kikushi
- Kioromo (zaidi ya 48 milioni pamoja na Ethiopia)
- Kiborana, 276,000 (2019)
- Kiorma, 92,000 (2019)
- Kisomali 2.8 milioni (27 milioni pamoja na Ethiopia and Somalia)
Dini
[hariri | hariri chanzo]Ukristo ndio dini kubwa zaidi nchini Kenya ambapo asilimia 85.5 ya watu wanajitambulisha kama Wakristo. 11% ya Wakenya ni waislamu hasaa maeneo ya Kaskazini mashariki mwa Kenya na pwani.2% Hawana dini yoyote
- Ukristo - 85%
- Ukristo wa Kiprotestanti – 33.4%
- Ukristo wa Kikatoliki – 20.6%
- Makanisa ya Kiinjili – 20.4%
- Makanisa ya Kiafrika – 7%
- Uislamu – 11%
- Uhindu, Usikh, na dini nyingine – 1.5%
- Watu wasio na dini– 2%
Miji na Ukuaji wa miji
[hariri | hariri chanzo]Kenya ina idadi chache ya wanaoishi miji ila inaongezeka kwa kasi. Asilimia 29% ya Wakenya ndio wanaoishi mijini.
- 1. Nairobi – watu milioni 4.3
- 2. Mombasa – watu milioni 1.2
- 3. Kisumu – watu 600,000
- 4. Nakuru – watu 570,000
- 5. Eldoret – watu 475,000
Ukuaji wa miji unasababishwa na uchumi unaokua, fursa za ajira, na miundombinu bora, lakini pia kuna changamoto kama msongamano, ukosefu wa ajira, na uhaba wa makazi bora.
Afya
[hariri | hariri chanzo]Kulingana na Kiashiria cha Huduma za Afya Kenya ndio nchi ya pili kwa ubora wa huduma za afya baada ya Afrika Kusini. [6]. Kenya imepiga hatua kubwa katika sekta ya afya kupitia upanuzi wa bima ya afya ya kitaifa , ambayo imeongeza upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi wengi, hasa wale wa kipato cha chini. Vilevile, serikali imewekeza katika ujenzi wa hospitali za kisasa na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, hivyo kuboresha ubora wa huduma za afya nchini.
Umri wa Kuishi
[hariri | hariri chanzo]Matarajio ya maisha nchini Kenya yanaendelea kuongezeka kutokana na uboreshaji wa huduma za afya na udhibiti wa magonjwa.
- Umri wa kuishi (2024): miaka 67.8
- Wanaume: miaka 65.4
- Wanawake: miaka 70.2
Changamoto kubwa za kiafya ni malaria, UKIMWI, maambukizi ya njia ya upumuaji, na matatizo ya uzazi. Serikali imewekeza katika mpango wa bima ya afya kwa wote ili kuboresha huduma za afya.
Kiwango cha Uzazi
[hariri | hariri chanzo]Wastani wa watoto wanaozaliwa na mwanamke mmoja nchini Kenya umepungua kwa sababu ya elimu bora, upangaji uzazi, ukuaji wa mijini pamoja na ugumu wa uchumi.
- 1960 – watoto 7.4 kwa kila mwanamke
- 1990 – watoto 5.4 kwa kila mwanamke
- 2010 – watoto 4.6 kwa kila mwanamke
- 2024 – watoto 3.4 kwa kila mwanamke
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Watoto huhudhuria shule ya chekechea hadi wanapofikia umri wa miaka mitano. Hii huchukua kati ya mwaka mmoja hadi mitatu (KG1, KG2 na KG3) na hufadhiliwa kibinafsi kwa sababu hapakuwa na sera ya serikali kuhusu elimu ya awali hadi hivi karibuni.
Elimu ya msingi ya kawaida huanza wakiwa na umri wa miaka sita na huchukua jumla ya miaka 12, ikijumuisha miaka minane ya shule ya msingi na miaka minne ya shule ya upili au sekondari. Shule ya msingi ni bure katika shule za umma, na wanafunzi wanaomaliza wanaweza kujiunga na vyuo vya ufundi vya vijana au polytechnic za vijijini, au kupanga mafunzo ya kujifunza kazi kama ushonaji, useremala, urekebishaji wa magari, uashi, na ujenzi kwa muda wa takriban miaka miwili.
Wanafunzi wanaomaliza shule ya upili wanaweza kujiunga na chuo cha ufundi au chuo cha kiufundi kwa muda wa miaka mitatu, au kuendelea moja kwa moja hadi chuo kikuu kwa muda wa miaka minne. Wahitimu kutoka vyuo vya ufundi na vyuo vya kiufundi wanaweza kuingia katika soko la ajira na baadaye kupata diploma ya juu maalumu baada ya mafunzo ya mwaka mmoja hadi miwili zaidi, au kujiunga na chuo kikuu—kwa kawaida wakianza mwaka wa pili au wa tatu wa kozi zao husika. Diploma ya juu inakubalika na waajiri wengi badala ya shahada ya kwanza, na katika baadhi ya vyuo vikuu, inaruhusu uandikishaji wa moja kwa moja au wa haraka katika masomo ya uzamili.
Asilimia 81 ya watu wazima wanaweza kusoma na kuandika. Serikali imefanya juhudi kubwa katika elimu kwa wote.
- Usajili wa shule za msingi: asilimia 96
- Usajili wa shule za sekondari: asilimia 68
- Wanafunzi wa vyuo vikuu: zaidi ya 2%
Kenya inatoa elimu ya msingi bila malipo na elimu ya sekondari kwa gharama nafuu, ingawa changamoto kama msongamano darasani na uhaba wa walimu bado zipo.
Uhamiaji
[hariri | hariri chanzo]Kenya ina idadi kubwa ya raia wake wanaoishi nje ya nchi, haswa katika Marekani, Uingereza, Kanada, na Australia. Pia, Kenya ni mwenyeji wa wakimbizi kutoka Somalia, Sudan Kusini, na Ethiopia, ikiwa na zaidi ya wakimbizi 700,000 walioandikishwa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 Worldometers. "Demographics of Kenya" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-03-20.
- ↑ Macrotrends. "Kiwango cha kuzaliwa cha Kenya" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-03-20.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 indexmundi. "Muundo wa Umri nchini kenya" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-03-20.
- ↑ KNBS. "Demografia za Kenya" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-03-10.
- ↑ Worldometers. "Kenya demographics" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-03-10.
- ↑ Statista. "Kiashiria cha Huduma za Afya" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-03-15.