Nenda kwa yaliyomo

Demi-Leigh Tebow

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Demi-Leigh Tebow

Demi-Leigh Tebow (alizaliwa Sedgefield, Western Cape, 28 Juni 1995) ni mwanamitindo, mwandishi, mwanaharakati wa kupinga biashara za binadamu, na mshindi wa mashindano ya urembo kutoka Afrika Kusini.

Anajulikana zaidi kwa kushinda taji la Miss Universe mnamo mwaka 2017. Kabla ya hapo, alitunukiwa taji la Miss South Africa mwaka 2017, na yeye ni mshindi wa pili wa Miss Universe kutoka Afrika Kusini, baada ya Margaret Gardiner, aliyeshinda taji hilo mwaka 1978.[1]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Demi-Leigh Nel-Peters alizaliwa na Bennie Peters na Anne-Marie Steenkamp. Alitambua nusu dada yake, Franje, aliyezaliwa akiwa na cerebellar agenesis, kama chanzo kikuu cha motisha katika maisha yake. Franje alifariki dunia 4 Mei 2019 akiwa na umri wa miaka 13.

Nel-Peters alihitimu kutoka North-West University mwezi Machi 2017, siku chache kabla ya kushinda Miss South Africa 2017. Anazungumza kwa ustadi Kiingereza na Kiafrikaans.

Zaidi ya mashindano ya Miss South Africa, Nel-Peters pia alishinda Miss Varsity Cup 2015 na kuwa miongoni mwa washindi watano bora (Top 5) katika Miss Teen SA 2010.[2][3]

  1. JK, Morne (27 Machi 2017). "Who is Demi-Leigh Nel-Peters". Jacaranda FM.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Miss South Africa Demi-Leigh Nel-Peters wins Miss Universe". CBS News (kwa American English). 26 Novemba 2017. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Denninger, Lindsay (26 Novemba 2017). "Miss South Africa Demi-Leigh Nel-Peters Wins Miss Universe 2017". Bustle.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Demi-Leigh Tebow kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.