Delfim Peixoto
Delfim de Pádua Peixoto Filho.(3 Januari 1941 - 28 Novemba 2016), anayejulikana kama Delfim Peixoto, alikuwa mwanasiasa wa Brazil na msimamizi wa soka ambaye alikufa kufuatia ajali ya Ndege ya LaMia Airlines. Wakati wa kifo chake alikuwa makamu wa rais wa Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) na rais wa Federação Catarinense de Futebol (FCF), nafasi ambayo alishikilia tangu 1985.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Delfim Peixoto alizaliwa mwaka 1941 huko Itajaí katika jimbo la kusini la Brazil la Santa Catarina. Alisoma sheria katika chuo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Santa Catarina. Akiwa mwanafunzi, Delfim Peixoto alikuwa mshiriki katika siasa za wanafunzi, akishiriki kama katibu wa Chama cha Wanafunzi wa Santa Catarina na kama mwanachama wa Chama kiKuu cha Wanafunzi wa Kitaifa.
Delfim Peixoto baadaye alitoa mihadhara katika sheria ya jinai na mazoezi ya kisheria katika Universidade do Vale do Itajaí.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Delfim Peixoto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |