Nenda kwa yaliyomo

Decameron (filamu)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

The Decameron (kwa Kiitalia: Il Decameron) ni filamu ya mwaka 1971 ya anthology iliyoandikwa na kuongozwa na Pier Paolo Pasolini, ni tafsiri ya hadithi za karne ya 14 zilizoandikwa na Giovanni Boccaccio.

Filamu hii ni ya kwanza katika mfululizo wa "Trilogy of Life" wa Pasolini, ikifuatiwa na The Canterbury Tales ya mwaka 1972 na Arabian Nights ya mwaka1974.

Kila filamu katika mfululizo huu inachukua kazi ya fasihi ya kale na kuielezea kwa mtazamo wa kisasa, ikilenga mada za ucheshi, ngono, na ukosoaji wa dini.

Pasolini hakulenga kuwasilisha kwa uaminifu ulimwengu wa Boccaccio, bali alitumia hadithi hizo kama njia ya kukosoa jamii ya kisasa kupitia sitiari[1]

Alibadilisha mazingira ya hadithi nyingi kutoka Firenze hadi kusini mwa Italia, hasa Napoli, na kutumia lahaja ya Neapolitan kuonyesha unyonyaji wa kiuchumi na kijamii wa maeneo maskini na yale tajiri kaskazini mwa Italia.

Filamu hii ilishinda Tuzo ya Dubu wa Fedha ya Heshima Maalum ya Majaji katika Tamasha la 21 la Kimataifa la Filamu la Berlin. [2]

  1. "Decameron Web | Arts".
  2. http://www.berlinale.de/en/archiv/jahresarchive/1971/03_preistr_ger_1971/03_Preistraeger_1971.html
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Decameron (filamu) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.