Deborah Adetuni Egunyomi
Deborah Adetuni Egunyomi (alizaliwa 10 Desemba 1953) ni profesa wa Elimu Endelevu na Isiyo Rasmi ndani ya Chuo Kikuu cha Ibadan, Ibadan, nchini Nigeria, [1] wakati huko nyuma alifanya kazi kama Mkuu wa Idara ya Elimu ya Watu Wazima. Alipata nafasi ya kuwa mjumbe wa Jopo la Ziara lililoanzishwa na serikali ya jimbo la Ekiti ili kuleta mageuzi kwenye nafasi ya Chuo cha Sayansi na Teknolojia ya Afya, Ijero-Ekiti . [2]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Mahali alipozaliwa Egunyomi ni mahali panapoitwa Ikole-Ekiti, Jimbo la Ekiti, Nigeria, kwa wazazi wake David na Esther Famoroti. Alipata masomo yake ndani ya Shule ya Methodist, Ikole-Ekiti, mnamo 1959– mamo 1964 kwa lego la elimu yake ya msingi, Shule ya Sarufi ya Wasichana ya Saint Mary kwa lengo la masomo ya sekondari kati ya mamo 1964 na mnamo 1970, na chuoni alihudhuria Chuo cha Elimu cha Jimbo la Kwara, Ilorin, mnamo 1974 hadi mnamo 1977. Kisha hapo mbeleni alihudhuria Chuo Kikuu cha Ibadan kwa ajili ya elimu yake ya Shahada yake ya Kwanza ya Sayansi (BS) kati ya mwaka wa 1980 na mwaka wa 1983, kabla ya kupata Shahada ya Uzamili ya Uhandisi wa Elimu (M.Ed) katika Mipango ya Elimu mwaka 1984 na Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) mnamo 1986. [3]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Kwenye mwaka wa 1986, Egunyomi alianza kazi yake rasmi ya kitaaluma ndani ya Chuo Kikuu cha Ibadan kwa nafasi ya msaidizi wa shahada ya uzamili. Alibobea juu ya masomo ya upembuzi yakinifu kwa lengo la kuanzishwa kwa Programu ya Mafunzo ya Nje, ambayo sasa ni Kituo cha Kujifunza kwa Umbali, cha Chuo Kikuu cha Ibadan. [ <span title="This claim needs references to reliable sources. (March 2024)">nukuu inahitajika</span> ]
Alifanikiwa kupata nafasi ya kuwa mhadhiri mnamo 1992, tena akaja kuwa mhadhiri mkuu mnamo 1995, kisha akafanikiwa kuwa profesa mnamo 2009. Alishika nafasi ya Kaimu Mkuu wa Idara ya Elimu ya Watu Wazima kati ya mnamo wa Februari 2010 na mnamo wa Januari 2012 na baadaye aliteuliwa tena kama Mkuu wa Idara mwaka wa 2014. [4]
Alivyofanikiwa kushika nafasi ya kuwa profesa wa kwanza mwanamke kwenye Idara ya Elimu ya Watu Wazima, Egunyomi alizungumza Hotuba ya Uzinduzi ya tano ya mwaka kwa mwaka kwenye Chuo Kikuu cha Ibadan kwenye tarehe ya 2 Julai 2015. [5] Alihudumu kama mtahini wa nje katika Vyuo Vikuu vingi vya Nigeria na Vyuo Vingi vya Elimu vya Nigeria katika ngazi za shahada ya kwanza na shahada ya uzamili. Amehudumu kama mshauri kwa mashirika ya kitaifa na kimataifa kama vile UNICEF, UNESCO, UNDP, mashirika ya serikali ya shirikisho, na mashirika yasiyo ya kiserikali. [ <span title="This claim needs references to reliable sources. (March 2024)">nukuu inahitajika</span> ]
Pamoja na hayo alifanya kazi kama mtahini wa nje ndani Chuo Kikuu cha Legon, Ghana, kuanzia mnamo wa 2007 hadi mnamo wa 2012. Aliteuliwa kama mjumbe wa Jopo la Ziara la EKSG la Kuteua Chuo cha Sayansi na Teknolojia ya Afya, Ijero-Ekiti na Gavana wa Jimbo la Ekiti, Dkt. Kayode Fayemi. [6]
Mikutano na machapisho
[hariri | hariri chanzo]Egunyomi alishiriki semina na warsha tofauti tofauti za ndani ya nchi na za kimataifa, mfano Warsha ya Kitaifa kuhusu Programu za Elimu Endelevu katika Kitivo cha Elimu cha Nigeria iliyofanyika ndani ya Chuo Kikuu cha Ibadan kwenye tarehe 10- tarehe 12 Septemba 1990; Mkutano wa nne wa Mapitio ya Mawaziri wa E9 uliofanyika Beijing, China, mnamo tarehe 22-23 Agosti 2001; Mkutano wa Kitaifa wa Mwaka wa Baraza la Kitaifa la Elimu ya Watu Wazima la Nigeria (NNCAE) 2008 uliofanyika Minna, Jimbo la Niger, Nigeria, Novemba 2008; na Mkutano wa tano wa Dunia kuhusu Elimu ya Mazingira uliofanyika Montreal, Kanada, Aprili 2009. [7]
Egunyomi alifanikiwa kuchapisha zaidi ya nyenzo 80 ndani na nje ya nchi, ikiwa ni jumuishi na sura za vitabu, makala za jarida, karatasi za mikutano, ripoti za kiufundi, vitabu, na monografu. [ <span title="This claim needs references to reliable sources. (March 2024)">nukuu inahitajika</span> ]
Familia
[hariri | hariri chanzo]Amefunga ndoa na Bwana Adeyemi Egunyomi, profesa mstaafu wa mimea.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "PROFESSOR Deborah Egunyomi | fresh news and views" (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-06-06. Iliwekwa mnamo 2020-06-06.
- ↑ "EKSG Appoints Visitation Panel for College of Health Science and Technology, Ijero-Ekiti – Ekiti State Website" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-06-06.
- ↑ Egunyomi, Professor Deborah. "Curriculum Vitae" (PDF). University of Ibadan.
- ↑ "Prof Michael Omolewa Delivers Inspiring Lecture As Adult Education Dept, UI Turns 70". Prompt News (kwa American English). 2019-10-02. Iliwekwa mnamo 2020-06-06.
- ↑ Egunyomi. "Balancing Life Equation with Continuing Education" (PDF). University of Ibadan.
- ↑ "EKSG Appoints Visitation Panel for College of Health Science and Technology, Ijero-Ekiti – Ekiti State Website" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-06-06."EKSG Appoints Visitation Panel for College of Health Science and Technology, Ijero-Ekiti – Ekiti State Website". Retrieved 6 June 2020.
- ↑ "EKSG Appoints Visitation Panel For College Of Health Science And Technology, Ijero-Ekiti – Ekiti State Website" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-06-18.