Dayosisi ya Kianglikana ya Mpwapwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Dayosisi ya Kianglikana ya Mpwapwa ni moja kati ya dayosisi 29 za Kanisa Anglikana Tanzania. Makao makuu yako mjini Mpwapwa.

Dayosisi hiyo ilianzishwa rasmi tarehe 23 Januari 1991, hadi wakati ule maeneo yake yalikuwa sehemu ya Dayosisi ya Tanganyika Kati. Askofu wa kwanza alikuwa Simon E. Chiwanga aliyehudumia hadi kustaafu mwaka 2007. Aliyemfuata kuwa askofu ni Jacob Chimeledya tangu 30 Septemba 2007.

Makao makuu ya dayosisi huwa na idara nne za Uinjilisti na Misioni, Elimu ya Kikristo, Fedha na Miradi ya Maendeleo.

Idadi ya Wakristo ni takriban 150,000 waliopo katika parokia 85 zenye sharika ndogo 680. Wanahudumiwa na makasisi 88 na madikoni 26 (idadi zote za mwaka 2009).[1]</ref>.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Diocese of Mpwapwa, tovuti binafsi ya familia Talings, iliangaliwa Mei 2021
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dayosisi ya Kianglikana ya Mpwapwa kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.