Dayo Amusa
Dayo Amusa (alizaliwa 20 Julai 1983) ni mwigizaji, mwimbaji, mtangazaji wa televisheni na mfanyabiashara kutoka Nigeria. Anajulikana sana kwa uigizaji wake katika filamu za Nollywood hasa filamu za Kiyoruba.[1][2][3]
Maisha ya Awali na Kazi
[hariri | hariri chanzo]Dayo alizaliwa Lagos, Nigeria.[4] Yeye ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watano. Mama yake anatokea Jimbo la Ogun huku baba yake akiwa anatokea Lagos. Alisoma katika Shule ya Mayflower, Ikenne. Dayo alisomea Sayansi na Teknolojia ya Chakula katika Chuo cha Ufundi cha Moshood Abiola kabla ya kuanza taaluma yake ya uigizaji mwaka 2002. Dayo alifanya utayarishaji wake wa kwanza mwaka 2006. Ingawa mara nyingi huigiza katika filamu za Lugha ya Kiyouruba ndani ya Nollywood, pia ameigiza katika filamu za lugha ya Kiingereza.[5][6][7] Dayo ni Mmiliki na Mkurugenzi wa Shule ya PayDab ambayo ina matawi mawili, moja likiwa Ibadan na jingine Lagos.[8][9]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nollywood Actress Dayo Amusa Drops New Single 'Blow My Mind'". Bella Naija.
- ↑ "DAYO AMUSA GIVES FREE SUMMER COACHING CLASS". Nigeria Films. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-23. Iliwekwa mnamo 2025-09-27.
- ↑ "Marriage is no shopping mall ― Dayo Amusa". Vanguard News (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2020-11-28. Iliwekwa mnamo 2022-07-19.
- ↑ "Dayo Amusa Biography, Career, Marriage, Age, Net Worth". Naijabiography Media (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-07-23.
- ↑ "My relationship with Mike Ezuruonye — Nollywood actress Dayo Amusa". The Nation.
- ↑ Aiye Jobele; Aje Egbodo. "I Missed Fatherly Care —Dayo Amusa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-24. Iliwekwa mnamo 2015-08-10.
- ↑ "Nollywood Actress Dayo Amusa Drops New Single".
- ↑ "Dayo Amusa opens nursery school in Ibadan, Oyo State". Niger Gists. Iliwekwa mnamo Agosti 10, 2015.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Gbenga Bada (Mei 27, 2015). "Actress hosts 5000 kids and rewards lucky winner with N100K". The Pulse. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2025-09-27.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dayo Amusa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |