Nenda kwa yaliyomo

David Stove

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

David Charles Stove (15 Septemba 19272 Juni 1994) alikuwa mwanafalsafa wa Australia ambaye maandishi yake mara nyingi yalipinga mitazamo ya kitaaluma iliyokubalika. Alijulikana kwa ukosoaji wake wa falsafa baada ya ukoloni, harakati za Ufeministi, na wazo la tamaduni mchanganyiko.

David Stove alibobea katika falsafa ya sayansi. Alikosoa hoja za wanafalsafa maarufu kama Karl Popper, Thomas Kuhn, Imre Lakatos na Paul Feyerabend, akidai mitazamo yao ilisababisha wasiwasi usio na tija kuhusu uhalali wa sayansi. Katika kitabu chake The Rationality of Induction (1986), alitoa hoja ya kutetea mantiki ya uhusishaji. Kwenye maandiko yake kama The Plato Cult and Other Philosophical Follies, alionyesha njia nyingi ambazo akili za binadamu hudanganyika, na alibuni neno “Horror Victorianorum” akimaanisha chuki ya kupitiliza kwa tamaduni na sanaa za enzi hizo. Stove alipinga nadharia ya sociobiology(taaluma ya sayansi inayochunguza jinsi tabia za kijamii za wanyama na wanadamu zinavyoathiriwa na biolojia, hasa urithi wa vinasaba (genes) na mageuzi) akiiita kama dini mpya. Katika maandiko yake alidai wanawake kwa ujumla wana uwezo mdogo wa kiakili kuliko wanaume, jambo lililozua utata mkubwa. Alifariki mwaka 1994."[1][2]

  1. Stove, David (1990). "The intellectual capacity of women". Proceedings of the Russellian Society. 15: 1–16.
  2. Also see Kimball, Roger (1997). "Who was David Stove?", The New Criterion 17, p. 21; Teichman, Jenny (2001). "The Intellectual Capacity of David Stove", Philosophy 76, pp. 149–57.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu David Stove kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.