David Ospina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ospina

David Ospina Ramírez (alizaliwa tarehe 31 Agosti 1988) ni mchezaji wa soka wa Colombia ambaye anacheza kama golikipa wa timu ya Arsenal FC, na timu ya taifa ya Colombia.

Ospina alianza kazi yake na Atlético Nacional mwaka 2005. Baada ya kiwango chake kukua, Ospina alijiunga na klabu ya Ufaransa Nice. Mwaka 2014, alijiunga na Arsenal kwa mkataba wa miaka minne.

Ospina amekuwa akiwakilisha nchi yake katika ngazi mbalimbali za kimataifa tangu mwaka 2007. Alikuwa golikipa wa pili mdogo zaidi kuchezea timu ya taifa ya Colombia. Amewahi kucheza takriban mechi 90 kwa taifa lake, Pia aliisaidia Colombia katika kombe la Dunia la FIFA 2018 kufika mpaka hatua ya kumi na sita bora.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu David Ospina kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.