Nenda kwa yaliyomo

David Ginola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
David Ginola Deauville 2014

David Ginola-Ceze (alizaliwa 25 Januari 1967) ni mchezaji wa zamani wa soka la kulipwa kutoka Ufaransa. Pia amewahi kufanya kazi kama mtangazaji wa televisheni, mwigizaji, mwanamitindo na mchambuzi wa soka.

Alicheza katika nafasi ya mshambuliaji. Alitumia misimu kumi nchini Ufaransa akiichezea Toulon, Racing Paris, Brest na Paris Saint-Germain.

Mwezi Julai 1995, alihamia Newcastle United katika ligi ya English Premier League. Baadaye aliichezea pia Tottenham Hotspur, Aston Villa na Everton, kabla ya kustaafu kucheza soka mwaka 2002.

Katika ngazi ya kimataifa, Ginola aliichezea timu ya taifa ya Ufaransa kati ya 1990 na 1995, akicheza jumla ya mechi 17 na kufunga mabao 3.[1][2]

  1. ↑ https://www.tottenhamhotspur.com/the-club/history/legends/david-ginola
  2. ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2026-04-21. Iliwekwa mnamo 2026-08-08.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu David Ginola kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.