Darine Stern
Darine Stern (16 Novemba 1947 – 5 Februari 1994) [1] alikuwa mwanamitindo wa Marekani na mwanamitindo wa kwanza Mwafrika-Amerika aliyeonekana kwenye jalada la jarida la Playboy peke yake katika toleo la Oktoba mwaka wa 1971..
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Muonekano wake ulifuata ule wa Jean Bell, ambaye aliangaziwa kwenye jalada la jarida hilo la mnamo Januari mwaka wa 1970 pamoja na wanamitindo wanne weupe.
Alianza kazi yake mwishoni mwa miaka ya 1960 kama mfanyakazi wa benki na pia alikuwa mfanyakazi wa mgahawa wa Top of the Hancock Building. Huko alipata mashabiki mbalimbali maarufu na kukutana na mume wake ambaye ni, David Ray. [2] Wakati alipokuwa mfanyakazi wa benki,na mpiga picha alitembelea benki yake aliomba kumpiga picha. Picha alizopiga zilifikia umakini wa timu ya wahariri ya Playboy, jambo lililomfanya achaguliwe na kuonekana kwenye jalada la jarida hilo.
Baada ya kuolewa na Ray, alikuwa mke wa daktari wa meno, na alikuwa mama wa kambo wa mtoto wa Ray, kisha akaenda New York City kuendeleza taaluma ya uanamitindo, yeye na Ray walipeana talaka.
Baada ya kuonekana kwenye jalada la Play Boy, aliendelea kuwa mwanamitindo maarufu, akiwakilishwa na wawamitindo wa itwao Ford Models Nina Blanchrd,Ellen Harth na Shirley Hamilton Models wa jijini Chikago na New York, na hata baadhi ya maonyesho ya Nchini Uingereza.Alirudi Chicago kwenda kufanya kazi kama mkurugenziwa mitindo,mshauri wa picha na mbunifu wa mavazi.
Alianzisha Darine Stern Agency ili kukuza kazi za wanamitindo wanaoanza shughuli za mitindo. [3] Mwanzoni mwa miaka ya 1990 Darine alihamia Martha's Vineyard, Massachusetts na alikuwa na uhusiano na kiongozi wa biashara Mwafrika-Amerika Kenton Clarke .
Alifariki mnamo tarehe 5 Februari, mwaka wa 1994, kutokana na ugonjwa wa saratani ya matiti.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Social Security Death Index [database on-line]". The Generations Network. Iliwekwa mnamo Oktoba 13, 2009.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ {{Rejea tovuti|author=Jerkins|first=Morgan|title=What Happened to Playboy's First Black Cover Girl?|url=https://zora.medium.com/what-happened-to-playboys-first-black-cover-girl-25f48b985edb|work=Zora|date=11 February 2020|publisher=Medium|accessdate=6 July 2020}
- ↑ Jerkins, Morgan (11 Februari 2020). "What Happened to Playboy's First Black Cover Girl?". Zora. Medium. Iliwekwa mnamo 6 Julai 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Jerkins, Morgan (11 February 2020). "What Happened to Playboy's First Black Cover Girl?". Zora. Medium. Retrieved 6 July 2020.