Daniel Bonjour

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Daniel Bonjour
Amezaliwa Septemba 28, 1981
Afrika Kusini
Kazi yake mwigizaji
Miaka ya kazi 2007–hadi sasa
Watoto 1

Daniel Bonjour (alizaliwa Septemba 28, 1981) ni mwigizaji na mwandishi wa filamu wa Afrika ya Kusini na anafahimika vema katika uhusika wake katika filamu ya The Walking Dead na iZombie.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Bonjour alizaliwa katika jiji la Johannesburg, Afrika ya Kusini.[1] Baba yake mzazi ni mhariri wa kulipwa na mkurugenzi anayetambulika kwa jina la Trevor Hill na mama yake ni raia wa Swiss. Walihamia Uswizi akiwa na umri wa miaka tano (5) na kurejea Afrika ya Kusini akiwa na umri wa miaka nane (8). Akiwa na miaka kumi na mbili (12), familia yake walihamia Seattle, Washington. Alihudhuria shule ya sekondari ya Mercer Island na kuhitimu katika chuo cha Boston.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Daniel alikuwa mhusika mkuu katika filamu yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka kumi na mbili (12) lakini hakuendelea na uigizaji hadi ilipofikia mwaka 2007 alipoanza kuwa mhusika mkuu katika filamu ya Indie na alitunikiwa tuzo ya mwigizaji bora kutoka International Academy of Web Television. Mwaka 2016 Daniel alitambulika kama Daniel Lawrence katika filamu za mwendelezo ya CW Frequency akiwa pamoja na Peyton List na Mekhi Phifer.[2] Daniel pia ni mwandishi na mshindi wa kwanza wa mashindano ya uandishi wa filamu mwaka 2015.[3] Alifanya kazi na baadhi ya michezo ya video zilizoshinda tuzo mbalimbali kama vile Hitman, Final Fantasy na Life is Strange.[4]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Daniel amemuoa mwigizaji Jelly Howie.[5][6] Wanamtoto mmoja wa kiume kwa jina Brixton Riot Bonjour.[7] Daniel anakaka mmoja aitwaye Pascal anayeishi Seattle, walipo wazazi wake. Alilazimika kukatiza fungate lake na Jelly Howie nchini Thailand na kuelekea Atlanta kuigiza filamu ya The Walking Dead.[8] Daniel alikuwa miongoni mwa waigizaji bora chipukizi wa kuwaangalia Hollywood kutokana na jarida la People.[9]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Jina Uhusika! Muongozaji
2008 Midnight Movie Josh Jack Messit
2009 Dragonquest Arkadi
2013 Ambushed Frank Giorgio Serefino
2016 After the Rain Ryan Daniel Bonjour
2021 Venus as a Boy Johnny Ty Hodges

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Five Things You Didn't Know About Daniel Bonjour". 18 October 2017.  Check date values in: |date= (help)
  2. "Hollywood's Hottest Up-and-Comers Hit PEOPLE's Ones to Watch Party: See the Pics!". 
  3. "Our Big Break Was Exactly That... - Final Draft®". 21 June 2016.  Check date values in: |date= (help)
  4. "Daniel Bonjour (visual voices guide) - Behind The Voice Actors". Behind The Voice Actors. Check mark indicates role has been confirmed using screenshots of closing credits and other reliable sources. 
  5. "Five Things You Didn't Know About Daniel Bonjour". 18 October 2017.  Check date values in: |date= (help)
  6. "Daniel Bonjour – iZombie". 23 April 2018.  Check date values in: |date= (help)
  7. https://www.instagram.com/p/BnzBK1InwW8/
  8. RAPP, ILANA (2016-12-13). "The CW's Frequency Actor Daniel Bonjour's Dishes on 'Daniel and Raimy'". Huffington Post (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2018-05-16. 
  9. "Hollywood's Hottest Up-and-Comers Hit PEOPLE's Ones to Watch Party: See the Pics!". 
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Daniel Bonjour kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.