Nenda kwa yaliyomo

Mbwigu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Corvinella)
Mbwigu
Mbwigu barabara
Mbwigu barabara
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Corvoidea (Ndege kama kunguru)
Familia: Laniidae (Ndege walio na mnasaba na mbwigu)
Jenasi: Corvinella Lesson, 1831

Eurocephalus A. Smith, 1836
Lanius Linnaeus, 1758
Urolestes Cabanis, 1850

Spishi: Angalia katiba.

Mbwigu ni ndege wakubwa kiasi wa familia Laniidae. Wanatokea Afrika, Asia na Ulaya kwa muhimu, spishi mbili tu huzaa huko Amerika ya Kaskazini. Ndege hawa ni mweusi na mweupe kwa kawaida, mara nyingi wana rangi ya kijivu, kahawa na nyekundu pia. Wana domo nene lenye ncha kwa kulabu na spishi nyingi zina mkia mrefu. Hula wadudu na vertebrata wadogo (mijusi, panya, ndege n.k.) na huwa na tabia ya kuwafumia mwiba. Mwiba unafaa kama akiba na ili kushikilia windo wakati mbwigu akichana vipande. Hulijenga tago lao kwa vijiti na nyasi mtini au kichakani. Jike huyataga mayai 3-9.

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]