Conor Bradley

Conor Bradley (alizaliwa 9 Julai 2003) ni mchezaji wa kulipwa kutoka Ireland Kaskazini ambaye anacheza kama beki wa kulia wa klabu ya mpira wa miguu ya Liverpool F.C. na timu ya taifa ya Ireland Kaskazini.
Maisha yake binafsi na ya awali
[hariri | hariri chanzo]Conor Bradley[1] alizaliwa julai 9 2003 huko Castlederg, kaunti ya Tyrone,[2] alipolelewa na kukua. Aliichezea timu yake ya nyumbani ya Gaelic,Aghyaran St Davog, na kipaji chake kuonekana toka alipokuwa mdogo.[3] Alisoma shule ya Christian Brothers Grammar School huko Omagh, na kusimamiwa haraka ilikumaliza kozi yake ya mtaala wa GCSE.[4] Baba yake Joe Bradley, alifariki nyumbani huko Killen, kaunti Tyrone, Februari 2024, baada ya kipindi kirefu cha kuugua.[5]
Vilabu alivyopitia
[hariri | hariri chanzo]Liverpool
[hariri | hariri chanzo]Hapo mwanzoni
[hariri | hariri chanzo]Bradley alianza maisha yake ya ujana akiwa na klabu ya nyumbani ya St Patrick akiwa na umri wa miaka tisa na pia alianza mazoezi katika kituo cha maendeleo cha klabu ya Liverpool ya Uingereza huko Ireland Kaskazini akiwa na umri huo huo.[6][7] Aliendelea kuchezea timu za Dungannon United Youth na Dungannon Swifts, kabla ya kuhamia England kujiunga na akademia ya vijana ya Liverpool mnamo mwaka 2019 kwa mkataba wa masomo wa miaka miwili. Hata hivyo, baada ya kukaa klabuni hapo kwa mwaka mmoja, alisaini mkataba wake wa kwanza na Liverpool, uliokuwa na muda wa miaka mitatu mpaka kufikia mwaka 2023.[8]
Bradley alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha kwanza cha Liverpool mnamo Septemba 2021 kwenye mchezo wa EFL Cup dhidi ya Norwich City. Kwa kufanya hivyo, akawa mchezaji wa kwanza kutoka Ireland ya Kaskazini kuchezea Liverpool katika mechi ya ushindani tangu wakati wa Sammy Smyth mnamo mwaka 1954.[9]
Mkopo kwenda Bolton Wanderers
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Juni 21 2022, Bradley alitia saini na timu ya daraja la kwanza ya Bolton Wanderers kwa mkopo wa msimu mzima.[10] Aliichezea timu hio kwa mara ya kwanza Julai 30 katika mechi iliyoisha kwa sare ya 1-1 wakiwa ugenini dhidi ya klabu ya Ipswich Town F.C.[onesha uthibitisho] Alifunga goli lake la kwanza wakicheza dhidi ya timu ya Salford City F.C katika kombe la EFL waliposhida magoli 5-1 Agosti 9.[11] Wiki moja baadae kuandika bao lake la kwanza la ligi, likiwa ndo goli pekee katika mechi hio dhidi ya Morecambe F.C waliposhinda 1-0.[12] Aprili 2 2023 Bradley alianza katika kikosi cha kwanza katika fainali ya EFL ambapo timu ya Boston ilipata ushindi wa 4-0 dhidi ya Plymouth Argyle F.C.[13] Aprili 29, alianza katika kikosi cha kwanza ambacho kilishinda ushindi wa 2-0 dhidi ya Fleetwood Town F.C, ushindi huo ulioipeleka timu ya Bolton hadi hatua mechi za kupnda daraja (Play-offs).[14] Siku hio hio jina lake likitajwa kwa kupigiwa kura na kushinda kuwa mchezaji bora wa Bolton Wanderers F.C kwa mwaka 2022–23 na pia alitunukiwa tuzo za Mchezaji Bora wa Mwaka (chaguo la wachezaji wenzake) na Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka, ambapo tuzo hiyo ya chipukizi aliipata kwa kushirikiana na James Trafford.[15][16]
Kurudi Liverpool: Msimu wa 2023–2024
[hariri | hariri chanzo]
Tarehe 21 Januari 2024, Bradley alicheza mechi yake ya kwanza ya Premier League katika ushindi wa 4-0 dhidi ya AFC Bournemouth,[17] alianza mechi kwa kutoa assist ya goli na kufanya kupatikana kwa goli la pili la Diogo Jota. January 31 alifunga goli lake la kwanza akiwa na Liverpool katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Chelsea F.C.[18] Pia alisajili pasi mbili za mabao, na kumfanya kuwa mchezaji bora wa mechi kwa mara ya pili ndani ya siku tatu.[onesha uthibitisho]
Tarehe 25 Februari 2024, Bradley alianza katika kikosi cha kwanza na kuichezea Liverpool akiwa beki wa kulia katika fainali ya Kombe la EFL 2024 dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Wembley, kabla ya kutolewa dakika ya 72. Liverpool waliendelea na ushindi wa bao 1-0 baada ya muda wa nyongeza, na kufanya Bradley kupata kombe lake la kwanza akiwa na klabu hiyo.[19]
Msimu wa 2024–2025
[hariri | hariri chanzo]Akiwa amejiimarisha vizuri kama mchezaji anaetumika mara kwa mara wakati wa msimu wa 2023-24 Liverpool, Bradley alipata sifa kubwa kwa mwanzo wake mzuri wa maisha ya mpira chini ya meneja mpya Arne Slot kipindi chake cha ukocha wa msimu wa 2024-25.[20]
Mechi iliyompa sifa zaidi ni miongoni mwa mechi ya klabu bingwa ulaya kati ya Liverpool na Real Madrid CF Novemba 27 2024, ambayo iliwapa ushindi wa 2-0 ulionyesha mchezo mkali wa kipindi cha kwanza kwa beki huyo dhidi ya fowadi wa Ufaransa Kylian Mbappé, na hivyo kumpa sifa kubwa beki huyo mchanga kwa kumdhibiti fowadi huyo vizuri sana.[21]
Liverpool ilishinda Ligi kuu Uingereza 2024-25, na kumfanya Bradley kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Ireland kutwaa taji hilo tangu Jonny Evans ambaye alishinda akiwa na Manchester United F.C katika 2013. Tarehe 17 Mei 2025, ilitangazwa kuwa Bradley ametia saini mkataba mpya wa muda mrefu na Liverpool. [22]
Tarehe 25 Februari 2024, Bradley alianza kuichezea Liverpool akiwa beki wa kulia katika kikosi cha kwanza katika fainali ya Kombe la EFL la 2024 waliyocheza dhidi ya Chelsea F.C. katika uwanja wa taifa wa Wembley, kabla ya kutolewa dakika ya 72. Liverpool wakiendelea na ushindi wa bao 1-0 baada ya muda wa majeruhi, na kumpatia Bradley kombe lake la kwanza akiwa na klabu hiyo.[19]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "2023/24 Premier League squad lists". Premier League. 13 Septemba 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Septemba 2023. Iliwekwa mnamo 14 Septemba 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Gates, Emmet (22 Septemba 2021). "Jürgen Klopp pleased with Conor Bradley as youngster ends 66-year Liverpool wait". Liverpool.com. Reach. Iliwekwa mnamo 2 Machi 2024.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Wilson, David (23 Januari 2024). "Liverpool FC's Conor Bradley 'did things no other child could'". BBC News. Iliwekwa mnamo 10 Februari 2024.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Gartland, Niall (24 Januari 2024). "The makings of a star". We Are Tyrone (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2026-05-21. Iliwekwa mnamo 5 Mei 2024.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Liverpool FC mourns passing of Conor Bradley's father". Liverpool F.C. 3 Februari 2024. Iliwekwa mnamo 3 Februari 2024.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
- Hewitt, Ralph (7 Februari 2024). "Funeral for father of Liverpool FC and NI star Conor Bradley takes place in Co Tyrone". Belfast Telegraph. Iliwekwa mnamo 10 Februari 2024.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "'A manager's dream': How Conor Bradley earned professional Liverpool contract after joining Academy aged nine". Belfast Telegraph. 2 Juni 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hanna, Gareth (26 Mei 2021). "Who is Conor Bradley? All you need to know about Liverpool star named in the Northern Ireland squad". Belfast Telegraph. Iliwekwa mnamo 30 Mei 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Youngster signs professional contract". Dungannon Swifts F.C. 1 Juni 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 30 Mei 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
- "Conor Bradley signs first pro contract with Liverpool FC". Liverpool F.C. 28 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 30 Mei 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Conor Bradley starts on Liverpool debut against Norwich in Carabao Cup as Northern Ireland's long wait is ended by Jurgen Klopp". Belfast Telegraph. Iliwekwa mnamo 21 Septemba 2021.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Wanderers Complete Conor Coup". Bolton Wanderers F.C. Iliwekwa mnamo 21 Juni 2022.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Bolton Wanderers 5–1 Salford City". BBC Sport. 9 Agosti 2022. Iliwekwa mnamo 10 Agosti 2022.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ McKendry, Adam (16 Agosti 2022). "Conor Bradley sends fans wild as he continues outstanding start to the season with another goal for loan side Bolton". Belfast Telegraph. Iliwekwa mnamo 16 Agosti 2022.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Pilnick, Brent (2 Aprili 2023). "Bolton Wanderers 4–0 Plymouth Argyle". BBC Sport. Iliwekwa mnamo 2 Aprili 2023.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Bolton Wanderers 2–0 Fleetwood Town". BBC Sport. 29 Aprili 2023. Iliwekwa mnamo 29 Aprili 2023.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Bradley Is Season Star". Bolton Wanderers F.C. 29 Aprili 2023. Iliwekwa mnamo 29 Aprili 2023.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Iles, Marc (30 Aprili 2023). "'We're not finished yet!' Prize guy Conor wants more glory in the play-offs". The Bolton News. Iliwekwa mnamo 5 Mei 2023.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nunez and Jota both strike twice in Liverpool victory at Bournemouth - Liverpool FC". Liverpool F.C. Januari 2024. Iliwekwa mnamo 22 Januari 2024.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Bradley shines as leaders Liverpool beat Chelsea". BBC Sport. Iliwekwa mnamo 31 Januari 2024.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 McNulty, Phil (25 Februari 2024). "Chelsea 0–1 Liverpool". BBC Sport. Iliwekwa mnamo 25 Februari 2024.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Conor Bradley: How Liverpool full-back has proved he can replace Trent Alexander-Arnold". 6 Februari 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Pearce, James (10 Desemba 2024). "Liverpool's Conor Bradley and a tackle for the ages". The New York Times.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Carroll, James (17 Mei 2025). "Conor Bradley signs new Liverpool FC Contract". Liverpool FC.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)