Conchita Wurst
Thomas Neuwirth (alizaliwa 6 Novemba 1988) ni mwimbaji, muigizaji, mtu maarufu kwenye vyombo vya habari, na drag queen (mwanaume anayevaa na kuigiza kama mwanamke) kutoka Austria ambaye anajulikana kwa jina lake la jukwaani la Conchita Wurst, akipewa jina la utani la 'Malkia wa Austria'. Alipata umaarufu wa kimataifa baada ya kushinda Shindano la Muziki la Eurovision mnamo mwaka 2014 kwa niaba ya Austria na wimbo wa Rise Like a Phoenix'.[1][2]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Neuwirth alizaliwa mnamo Novemba 6, 1988, huko Gmunden na alilelewa katika mji mdogo wa Bad Mitterndorf, kwenye maeneo ya mashambani ya Styria nchini Austria. Alieleza kuwa eneo hilo la milimani lilikuwa sehemu nzuri sana ya kukulia, lakini alikabiliwa na ubaguzi kwa kuwa shoga [3][4].
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 2006, Neuwirth alishiriki katika msimu wa tatu wa kipindi cha televisheni cha Austria kiitwacho Starmania, akimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Nadine Beiler. Mwaka mmoja baadaye, Neuwirth alianzisha bendi ya wavulana ya Jetzt Anders!, lakini kikundi hicho kilisambaratika ndani ya mwaka huo huo.[5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.politico.eu/article/conchita-wurst-eurovision-queen-austria/
- ↑ https://www.nytimes.com/2024/05/06/arts/music/conchita-wurst.html
- ↑ https://web.archive.org/web/20150525014439/http://conchitawurst.com/bio/
- ↑ https://www.thepinknews.com/2014/06/12/eurovision-winner-conchita-wurst-i-was-bullied-for-wearing-a-dress-to-school/
- ↑ https://wien.orf.at/v2/news/stories/2602913/
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Conchita Wurst kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |