Commonitorium

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Commonitorium[1] (jina hilo la Kilatini lilitumiwa naye kudokeza kwamba aliandika aweze kujikumbusha: ndiyo maana ya kichwa jicho) ni kitabu maarufu kilichoandikwa na Vinsenti wa Lerins mwaka 434 hivi, yaani miaka 3 baada ya Mtaguso wa Efeso.

Huyo mmonaki padri wa Galia (leo Ufaransa), akitaka kufanya imani ya Wakristo istawi ndani mwao, alikiandika akiwa katika monasteri ya Lérins kwenye kisiwa Saint-Honorat, na akitumia jina bandia la Peregrinus alibainisha vigezo vya kutofautisha ukweli wa imani sahihi uongo uliofichama katika uzushi.

Sawa na mtaguso mkuu huo, Vincent alitetea matumizi ya jina Mama wa Mungu kwa Bikira Maria, akipinga hoja za Nestori wa Konstantinopoli.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Commonitorium kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.