Cliff Simon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Cliff Simon
Amezaliwa 7 Septemba 1962
Johannesburg, Afrika Kusini
Amekufa 9 Machi 2021
Topanga, California, Marekani
Kazi yake Mwanamichezo

Cliff Simon (7 Septemba 19629 Machi 2021) alikuwa mwanamichezo na mwigizaji nchini Afrika ya Kusini, anajulikana hasa kutokana na nafasi yake kama Ba'al katika filamu ya Stargate SG-1.

Maisha ya mwanzo[hariri | hariri chanzo]

Simon alizaliwa Johannesburg, Afrika ya Kusini, mtoto wa nne wa Emmanuelle na Phylis Simon. Wazazi wake wote wawili walikuwa Wayahudi kutoka Poland na Lithuania.[1] Alipokuwa na umri mdogo, Simon alikuwa na ndoto za kuja kuwa mshindi wa kwanza mwogeleaji kutoka Afrika Kusini na kupata medali ya dhahabu ya Olimpiki. Alianza mazoezi mapema chini ya mwongozo wa mama yake, kama mwalimu wa kuogelea. Kwa umri wa miaka 6, alionyesha ujuzi katika mchezo wa sarakasi. Katika umri wa miaka 15, Simon alifikia kiwango cha kitaifa kama Mwogeleaji na Mwanasarakasi nchini Afrika Kusini , na aliacha mchezo wa sarakasi na kuzingatia katika kuogelea.[2][3]

Mwaka 1975, wazazi wa Simon waliamua kuhamia Ufalme wa Muungano, kutokana na machafuko barani Afrika. Huko ndipo Simon alihitimu shule na kuchaguliwa kuogelea kwenye timu ya kimataifa ya Uingereza. Alishinda kwenye majaribio ya olimpiki na kufuzu kwenye Olimpiki ya 1984 huko Los Angeles. Chuo Kikuu cha Houston na Southern Methodist University huko Texas vilimpa udhamini, ambapo alifanya mazoezi ya kuogelea na timu ya Marekani. Hii ingeweza kumpeleka kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka 1984. Hata hivyo, hakuingia kwenye mashindano.

Alirudi Afrika ya Kusini, na kujiunga na jeshi la anga akiendelea kuogelea na alishinda tuzo ya juu zaidi ya michezo iliyotolewa katika Air Force, Victor Ludorum.[1]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Kahla, Cheryl. "SA-born ‘Stargate’ and ‘Egoli’ actor Cliff Simon dies aged 58", The South African, 12 March 2021. Retrieved on 16 March 2021. 
  2. "'Stargate SG-1' actor Cliff Simon dies in kiteboarding accident", 12 March 2021. 
  3. "Cliff Simon death: Stargate SG-1 actor dies in tragic accident, aged 58", 12 March 2021. "‘He died doing one of the things he loved most,’ his wife said." 
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cliff Simon kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.