Ciudad Bolívar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kitovu cha kihistoria ya Ciudad Bolivar pamoja na daraja la Orinoco

Ciudad Bolívar ni mji mkuu wa jimbo la Bolivar katika Venezuela. Mji ulianzishwa 1764 kwa jina "Angostura" ukabadilishwa jina mwaka 1846 kwa heshima ya Simon Bolivar. Idadi ya wakazi ni 312,691 (mwaka 2000).

Mji ulianzishwa mahali ambako mto pana Orinoco ni nyembamba kiasi mwenye upana wa 1.6 km pekee. Hali hii iliwezesha kuvuka mto na kuanzisha mji ulioitwa awali kwa jina kamili 'Santo Tomé de Guayana de Angostura del Orinoco' ("Mt. Tomasi wa Guayana kwenye sehemu nyembamba wa Orinoco") yaani jina fupi "Angostura" lilimaanisha "sehemu nyembamba". Daraja la kwanza la mto Orinoco likajengwa hapohapo.

Leo hii mji ni kati ya vitovu vya kiuchumi vya beseni ya Orinoco.

Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ciudad Bolívar kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.