Nenda kwa yaliyomo

Citrus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chungwa tamu.

Citrus ni jenasi ya miti ya familia Rutaceae. Miti ya jenasi hiyo inazaa matunda machungwa, kama chenza, ambayo ni maarufu kwa harufu na ladha. Wakulima wamefaulu kuchanganya aina mbalimbali hadi kupata chungwa, limau na ndimu.

Asili yake ni Asia Kusini, Asia Mashariki, Asia Kusini-Mashariki, Melanesia, na Australia. Kilimo chake kilienea huko Mikronesia na Polinesia miaka 3000–1500 KK), halafu kwenye Mashariki ya Kati na Mediteranea (miaka 1200 KK) na hatimaye kutoka Ulaya hadi Amerika.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]