Chuo kikuu cha Pwani
Chuo Kikuu cha Pwani ni chuo kikuu cha umma [1] katika Kaunti ya Kilifi, Kenya, katika mji wa mapumziko wa Kilifi, kilomita 60 kaskazini mwa Mombasa. Kabla ya tuzo ya hati ya chuo kikuu, kilikuwa tawi la Chuo Kikuu cha Kenyatta. Chuo hicho, kilichokuwa Taasisi ya Kilimo ya Kilifi, ilianzishwa tarehe 23 Agosti 2007 kwa agizo lililotiwa saini na Rais Mwai Kibaki. [2]
Mahali
Chuo kikuu cha Pwani kinapatikana kwenye barabara kuu ya Mombasa-Malindi. Ni makazi katika takriban 239 hekta za ardhi, kweka nafasi ya upanuzi wa siku zijazo. Kundi la kwanza la wanafunzi katibia 200 lilisajiliwa tarehe 20 Oktoba 2007, hasa katika nyanja ya Elimu ya Sayansi na ya Sanaa. [3]
Shule zake
- Shule ya Elimu [4]
- Shule ya Binadamu na Sayansi ya Jamii [5]
- Shule ya Biashara na Uchumi [6]
- Shule ya Sayansi Safi na Inayotumika (SPAS) [7]
- Shule ya Sayansi ya Kilimo na Masomo ya Biashara ya Kilimo [8]
- Shule ya Sayansi ya Mazingira na Dunia [9]
- Shule ya Mafunzo ya Wahitimu (SGS) [10]
- Shule ya Afya na Sayansi ya Binadamu [11]
Utafiti
Chuo Kikuu cha Pwani kimetia saini Hati ya Maelewano, yanayogusa maeneo mbalimbali ya maslahi kama njia ya kuimarisha mwingiliano wa manufaa. [12] Chuo Kikuu kinashirikiana na taasisi za utafiti nchini Kenya na duniani kote. [13] Baadhi yao ni:
- Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Kenya ,
- Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya Ilihifadhiwa 18 Novemba 2022 kwenye Wayback Machine. ,
- Baraza la Taifa la Sayansi na Teknolojia ,
- Chuo Kikuu cha Jimbo la Florida ,
- Technische Universitat Dortmund [14]
- Chuo Kikuu cha Anglia Mashariki,
- Kituo cha John Innes nchini Uingereza,
- Chuo Kikuu cha Glasgow ,
- Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo
- Huduma ya Ukaguzi wa Afya ya Mimea Kenya.
- Chuo Kikuu cha Eldoret [15]
- Chuo Kikuu cha Sun Yet Sen [16]
Kwa ushirikiano na Baraza la Kitaifa la Sayansi na Teknolojia, chuo kikuu kilifanya kongamano la washikadau kushughulikia shida la utendaji duni katika masomo ya sayansi kwenye mitihani ya KSCE na viwango vya chini vya ubadilishaji kiwango kutoka ngazi yaawali ya shule ya msingi kuenda shule ya upili na Chuo Kikuu. [17]
Ili kufikia watu zaidi na ujumbe wa maendeleo katika kanda hili, chuo kikuu kimekuwa kikishiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Mombasa kutoka mwakwa wa 2008. Katika maonyesho haya ya biashara, chuo kikuu ina maonyesho ya matokeo ya utafiti wa kisayansi na ya teknolojia zilizotumika ambazo zinaweza kutumika na wakulima kutatua changamoto za uzalishaji wa kilimo, uhaba wa chakula na biashara za kilimo. [18]
Programu maalum
Ukanda wa pwani, kama sehemu nyingine nyingi za nchi ina changamoto ya VVU/UKIMWI na utumiaji mbaya wa Pombe na madawa ya kulevya. Wanafunzi wengi katika chuo kikuu ni vijana, katika umri hatari ya kuambukizwa VVU au kuangukia mtego wa matumizi ya madawa ya kulevya. Kwa kufahamu hatari hii, chuo kikuu kimeanzisha kitengo cha kudhibiti Ukimwi ambacho huratibu programu na shughuli za kupigana na changamoto za Ukimwi. kitengo hicho cha kudhibiti UKIMWI inaungwa mkono na kamati ya matumizi ya pombe na dawa za kulevya katika Chuo Kikuu. Kitengo hicho cha kudhibiti Ukimwi inapeana mafunzo kwa waelimishaji/washauri wanaotolewa kutoka kwa wanafunzi na kusambazwa katika kumbi za makazi na programu za masomo. Wanatambua kesi zinazoibuka na kutoa usaidizi kabla ya kupeleka kesi kwa washauri wa kitaalamu. Kila muhula kitengo cha kudhibiti Ukimwi hupanga wiki za VVU/UKIMWI kutoa huduma za ushauri nasaha na upimaji. Idara ya Sayansi ya Kibayolojia inapeana mafunzo kwa wanafunzi kuhusu ujuzi ili kuwasaidia wanafunzi katika miradi yao ya utafiti wa mwaka wa mwisho kama sehemu ya mtaala. Mafunzo haya ni ya ujifunzaji rika kwa wanafunzi na ni ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Pwani na Kituo cha The John Innes. [11]
Marejeo
- ↑ "Commission for University Education - Status Of Universities (Universities Authorized to Operate in Kenya) - Status Of Universities (Universities Authorized to Operate in Kenya)". www.cue.or.ke. Iliwekwa mnamo 2020-05-25.
- ↑ PU, Pwani University. Strategic Plan 2014-2024 (PDF). Pwani University. uk. 5.
- ↑ PU, Pwani University. Strategic Plan 2014-2024 (PDF). Pwani University. uk. 1.
- ↑ "Home". soe.pu.ac.ke. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-06-11. Iliwekwa mnamo 2020-05-30.
- ↑ "SHHS". shhs.pu.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2020-05-30.
- ↑ "School of Business and Economics". www.pu.ac.ke. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-06-22. Iliwekwa mnamo 2020-05-30.
- ↑ "SPAS". spas.pu.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2020-05-30.
- ↑ "SASA". sasa.pu.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2020-05-30.
- ↑ "SEES". sees.pu.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2020-05-30.
- ↑ "School of Graduate Studies". www.pu.ac.ke. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-06-22. Iliwekwa mnamo 2020-05-30.
- 1 2 "Pwani University". www.pu.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2020-05-15.
- ↑ "Strategic plan" (PDF). Pwani University. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2024-11-15. Iliwekwa mnamo 20 Februari 2024.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Collaborations". www.pu.ac.ke. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-06-20. Iliwekwa mnamo 2023-05-15.
- ↑ "Collaborations". Pwani University. 20 Septemba 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-06-22. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Collaborations". Pwani University. 20 Septemba 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-06-22. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Collaboration". Pwani University. 20 Septemba 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-06-24. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Pederson, Olivia (2025-05-17). "Beyond the Exam Score: An Examination of the Kenyan Education System, Its Reforms, Inefficiencies, and Impact on Individuals and Society at Large". Honors Projects.
- ↑ "Pwani University". www.pu.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2020-05-24.
Viungo vya nje
| Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chuo kikuu cha Pwani kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |