Chuo Kikuu cha Maseno
Chuo Kikuu cha Maseno kinapatikana katika mji wa Maseno, uliopo karibu umbali wa kilometa 30 Kaskazini Magharibi mwa jiji la Kisumu, Kenya. Chuo hiki kina matawi mawili makuu, yaani, Kampasi ya Kisumu na Kampasi Kuu (Main Campus). Kampasi kuu iko kando ya barabara ya Busia huku kampasi ya Kisumu ikiwa katika jiji la Kisumu. Ni moja ya vyuo vikuu saba vya Serikali nchini Kenya.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Chuo hiki kilianzishwa mnamo mwaka wa 1991 kama Chuo cha Maseno (Maseno University College) kutokana na muungano wa Siriba Teachers Training College na Government Training Institute chini ya Kifungu cha Sheria cha sheria,1991. Wanafunzi wa kwanza walisajiliwa mnamo Januari mwaka wa 1991. Chuo hiki kiligeuzwa kuwa Chuo Kikuu cha Maseno mnamo Januari 2001 kupitia Kifungu cha Sheria cha Maseno University cha mwaka 2000.[1]
Kozi
[hariri | hariri chanzo]Chuo Kikuu cha Maseno kinatoa mafunzo katika kozi zifuatazo:
- Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii
- Kitivo cha Elimu
- Shule ya Familia, Sayansi ya Matumizi na Teknolojia
- Taasisi ya Utafiti na Masomo ya Shahada ya pili (Postgraduate)
- Kitivo cha Sayansi
- Suluhisho kwa utafiti katika fani mbalimbali na ushauri wa Ziwa Victoria.
Matawi
[hariri | hariri chanzo]Kufikia sasa chuo hiki kina kampasi tatu:
Kampasi Kuu (Main Campus)
Chuo cha Siriba (Siriba University and College)[2] na
Kampasi ya Kisumu (Kisumu Campus) ambayo inapatikana jijini Kisumu na hutoa mafunzo ya Tarakilishi
Idadi ya Wanafunzi
[hariri | hariri chanzo]Chuo hiki kwa sasa kinakisiwa kuwa na idadi ya wanafunzi wapatao 250,000.[3]
Virejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ ^ Kuhusu Chuo Kikuu cha Maseno
- ↑ ^ Siriba Campus, Kutoka tovuti rasmi ya Chuo Kikuu cha Maseno, [1] Archived 18 Julai 2009 at the Wayback Machine.
- ↑ ^ Maseno University- Review and Web Ranking
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Maseno kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |