Nenda kwa yaliyomo

Christine Botlogetswe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Christine Ayanda Botlogetswe (alizaliwa tarehe 1 Oktoba 1995) ni mwanariadha wa mbio fupi kutoka nchni Botswana anayeshiriki zaidi katika mbio za mita 400.

Alishiriki katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016, ambapo alikimbia sekunde 52.37 katika duru ya kwanza, muda ambao haukumwezesha kufuzu kuendelea na mashindano.

Anawakilisha klabu ya Orapa Athletics Club na anafundishwa na kocha Justice Dipeba, ambaye pia ni kocha wa Isaac Makwala, mmoja wa wanariadha waliowahi kukimbia kwa kasi zaidi katika historia, akishika nafasi ya saba duniani. [1][2]

Botlogetswe pia alifuzu kuwakilisha Botswana katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya mwaka 2020.[3]

  1. "Rio 2016". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-21.
  2. "Olympics | Philly". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-09. Iliwekwa mnamo 2016-10-06.
  3. Sib, Anastacia; a (2021-06-16). "Botswana: Women Prove Point". allAfrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-06-19.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Christine Botlogetswe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.