Nenda kwa yaliyomo

Christian Tumi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kadinali Tumi.

Christian Wiyghan Tumi (15 Oktoba 19303 Aprili 2021) alikuwa mchungaji wa Kanisa Katoliki kutoka Kameruni ambaye alihudumu kama Askofu Mkuu wa Douala kutoka mwaka 1991 hadi 2009.

Alikuwa Askofu wa Yagoua kuanzia mwaka 1980 hadi 1982. Baada ya kuhudumu kama Askofu msaidizi wa Garoua kuanzia mwaka 1982, alikua Askofu wa Garoua kutoka mwaka 1984 hadi 1991.

Aliteuliwa kuwa kardinali mwaka 1988. Tumi alikuwa kardinali wa kwanza na hadi sasa ni kardinali pekee kutoka Kameruni.[1]

  1. Foute, Franck (3 Aprili 2021). "Décès de Christian Tumi, premier cardinal camerounais". Jeune Afrique (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 4 Aprili 2021.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.