Nenda kwa yaliyomo

Chihuahua (mbwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chihuahua kutoka Urusi, 2007

Chihuahua ni mbwa mdogo sana kutoka Mexico. Jina lake limetokana na jimbo la Chihuahua, na ni moja ya mbwa wadogo zaidi duniani.[1] Mara nyingi, watu humfuga kama mbwa wa nyumbani kwa urafiki.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Chihuahua mwenye kichwa cha swala ("deer-head") na manyoya mafupi
Mbwa Chihuahua aina ya apple-head kwa mtazamo wa upande
Chihuahua mwenye kichwa cha tofaa ("apple-head") na manyoya mafupi, akionyesha paji la uso lililochoropoka zaidi

Utafiti wa kinasaba unaonyesha kuwa mbwa wa asili wa Amerika waliingia kutoka Siberia miaka 10,000 iliyopita, na wakaishi huko bila kuingiliwa kwa miaka 9,000 hadi walipokutana na Wazungu wa kwanza. Mbwa hawa wa asili walikuwa na vinasaba vya kipekee ambavyo sasa karibu vimetoweka. Utafiti wa mwaka 2020 unaonyesha kuwa asilimia ndogo ya urithi huu wa asili bado upo kwa Chihuahua na mbwa mwingine wa Mexico, Xoloitzcuintli. Tafiti nyingine zinaonyesha kuwa asilimia ya urithi huu kwa Chihuahua inaweza kuwa hadi 70%.[2]

Kulingana na rekodi za kikoloni, mbwa wadogo sana walikuwepo katika eneo la Chihuahua mwanzoni mwa karne ya 19. Ripoti moja inasema kuwa wavamizi wa Kihispania wa karne ya 16 walikuta mbwa hawa wakiwa wengi sana.[3] Katika barua ya mwaka 1520, Hernan Cortés alisema kuwa Waazteki walifuga na kuuza mbwa wadogo kama chakula.[4]

Klabu ya Mbwa ya Marekani ilimsajili mbwa wa kwanza wa Chihuahua mnamo 1904, aitwaye Midget, ambaye alikuwa akimilikiwa na H. Raynor kutoka Texas.[5][6]

  1. "The 25 Smallest Dog Breeds". American Kennel Club. Iliwekwa mnamo 26 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. van Asch, Barbara; Zhang, Ai-bing; Oskarsson, Mattias C. R.; Klütsch, Cornelya F. C.; Amorim, António; Savolainen, Peter (2013-09-07). "Pre-Columbian origins of Native American dog breeds, with only limited replacement by European dogs, confirmed by mtDNA analysis". Proceedings of the Royal Society B: Biological Sciences. 280 (1766): 20131142. doi:10.1098/rspb.2013.1142. PMC 3730590. PMID 23843389.
  3. Pedro Baptista Pino y Juan Lopez Cancelada, Exposición sucinta y sencilla de la Provincia del Nuevo México y otros escritos. Ed. Jesus Paniagua Perez. Valladolid: Junta de Castilla / León: Universidad de León, 2007, p. 244: "Hata jangwani mbwa wadogo walikuwa wakipatikana, wakivinda panya, chura na mijusi." Kumbukumbu inayofuata inazungumzia wavamizi wa Kihispania waliokuwa na njaa wakila mbwa hawa (Universidad Veracruzana, Arquivo Viejo, XXVI.2711).
  4. "Hernan Cortés: from Second Letter to Charles V, 1520". Fordham University. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 23, 2014. Iliwekwa mnamo Machi 25, 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Coile, C. (2013). Chihuahuas: Everything about purchase, care, nutrition, behavior, and training. Hauppauge, NY: Barron's Educational Series, p. 7: "Ni mnamo mwaka wa 1904 ambapo American Kennel Club (AKC) ilisajili Chihuahua wake wa kwanza; jumla ya tano waliosajiliwa mwaka huo."
  6. "Chihuahua History: From Aztec Treasure to Popular Companion". American Kennel Club (kwa Kiingereza). Januari 6, 2022. Iliwekwa mnamo 2022-09-28.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)