Charles Young (mwanajeshi)
Mandhari
Charles Young (12 Machi 1864 – 8 Januari 1922) alikuwa mwanajeshi wa Marekani. Alikuwa mhitimu wa tatu Mwafrika-Mmarekani kutoka United States Military Academy, na alifanya historia kwa kuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza Weusi katika Jeshi la Marekani.
Alikuwa:
- Mkuu wa kwanza Mweusi wa hifadhi ya taifa ya Marekani
- Mwanajeshi wa kwanza Mweusi kuwa military attaché
- Mtu wa kwanza Mweusi kufikia cheo cha kanali katika Jeshi la Marekani
- Afisa Mweusi mwenye cheo cha juu zaidi katika Jeshi la kawaida la Marekani hadi alipofariki mwaka 1922
Mwaka 2022, kutokana na huduma yake ya kipekee na vikwazo vya ubaguzi wa rangi alivyokumbana navyo, alipandishwa cheo kwa heshima baada ya kifo chake na kuwa brigedia jenerali. Sherehe ya kumtukuza ilifanyika katika United States Military Academy huko West Point.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Duster, Chandelis (Aprili 29, 2022). [(https://www.cnn.com/2022/04/29/politics/charles-young-brigadier-general-us-army/index.html) "A century after his death, the first Black US Army colonel is promoted to brigadier general"]. CNN. Iliwekwa mnamo Aprili 30, 2022.
{{cite news}}: Check|url=value (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Charles Young (mwanajeshi) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |