Charles Messier

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Charles Messier

Charles Messier (tamka sharl mesye. *26 Juni 1730 – 12 Aprili 1817) alikuwa mwanaastronomia kutoka nchini Ufaransa anayekumbukwa kwa kutunga orodha ya magimba ya angani iliyojulikana kwa jina "Orodha ya Messier".

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa katika jimbo la Lorraine, Ufaransa. Alianza kuvutwa na habari za astronomia baada ya kuona nyotamkia kubwa ya mwaka 1744 na kupatwa kwa jua kwenye tarehe 25 Julai 1748.

Kazi yake ya kwanza kuanzia mwaka 1754 ilikuwa ajira kama karani wa Joseph Nicolas Delisle aliyekuwa mwanastronomia mkuu wa jeshi la maji la Ufaransa. Kazi ya Messier ilikuwa pamoja na kuchora ramani. Deslisle alitambua uwezo wake alimfundisha pia misingi ya astronomia. Hasa alimfundisha kuandika kila kitu alichotazama angani pamoja na maelezo makinifu.

Mwaka 1757 aliagizwa na Delisle kutafuta Kometi ya Halley iliyotabiriwa kurudi mwaka ule; aliitambua tu kwenye Januari 1759 kwa sababu utabiri ulikuwa na makosa. 1761 alitazama mpito wa Zuhura mbele ya jua na 1764 alifaulu kukuta nyotamkia wa kwanza asiyejulikana bado.

Tangu 1764 Messier alitafuta hasa nyotamkia angani. Kwa jumla alitambua 13 :[1]

 • C/1760 B1 (Messier)
 • C/1763 S1 (Messier)
 • C/1764 A1 (Messier)
 • C/1766 E1 (Messier)
 • C/1769 P1 (Messier)
 • D/1770 L1 (Lexell)
 • C/1771 G1 (Messier)
 • C/1773 T1 (Messier)
 • C/1780 U2 (Messier)
 • C/1788 W1 (Messier)
 • C/1793 S2 (Messier)
 • C/1798 G1 (Messier)
 • C/1785 A1 (Messier-Mechain)

Pamoja na nyotamkia hizi alikuta pia kiasi cha magimba mengine kama vile nebula, fungunyota au galaksi.

Tangu mwaka 1771 alianza kuzipeleka kwenye umma kwa njia ya orodha yake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Maik Meyer. Catalog of comet discoveries

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]