Charles Andler

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Charles Andler

Charles Philippe Théodore Andler (11 Machi 1866, Strasbourg1 Aprili 1933, Malesherbes, Loiret) alikuwa ni mwanafalsafa mwenye mchanganyiko wa Kijerumani na Kifaransa.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Andler alizaliwa katika familia ya kiprotestanti katika jiji la Strasbourg, nchini Ufaransa.[1] Mwaka 1887 hadi 1888, Andler alishindwa kufikia mafanikio ya juu katika falsafa, maamuzi yaliyofikiwa na Jules Lachelier. Lacheller alikuwa ni msimamizi na mkaguzi wa maswala ya falsafa, ambaye toka awali alionekana kuwa na mtazamo hasi juu ya falsafa ya Kijerumani. Baadae alibadilisha maamuzi ya kuchukua masomo ya falsafa ya Ujerumani suala lililompelekea kufaulu katika kiwango cha juu kabisa katika darasa lake. [2] Hatimaye Andler alifanikiwa kuwa profesa wa Kijerumani katika Sorbonne hii ikiwa mwaka 1901 na baadae chuo cha Collège de France mwaka 1926.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

  • Les origines du socialisme d'état en Allemagne, 1897
  • Collection de Documents sur le Pangermanisme, 4 vols, 1915–1917
  • Nietzsche, sa vie et sa pensée, 6 vols, 1920
  • Vie de Lucien Herr (1864-1926), 1932

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Antoinette Blum, 'Charles Andler (1866-1933)', in L'affaire Dreyfus: dictionnaire, 2006, p/117-120
  2. Robert Alun Jones, The development of Durkheim's social realism, Cambridge University Press, 1999

Masomo zaidi[hariri | hariri chanzo]

  • Ernest Tonnelat, Charles Andler: sa vie et son œuvre, 1937

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]