Nenda kwa yaliyomo

Chanjo ya matumbwitumwi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chanjo ya matumbwitumwi
Chanjo ya matumbwitumwi
Vaccine description
Target disease Mumps
Type Attenuated virus
Data ya kikliniki
MedlinePlus a601176
Kategoria ya ujauzito ?
Hali ya kisheria ?
Vitambulisho
Nambari ya ATC J07BE01
DrugBank <!—Data za kemikali--> <!—Data za kemikali-->
ChemSpider NAKigezo:Chemspidercite
 N(what is this?)  (thibitisha)

Chanjo ya matumbwitumwi inazuia ugonjwa wa matumbwitumbwi. Watu wengi wakichanjwa huwa inapunguza matatizo ndani ya jamii.[1] Inafaa zaidi kama asilimia 90% ya wananchi wakichanjwa na ubora wake unakadiriwa kuwa asilimia 85% ya wananchi.[2] Dozi mbili zinahitajika ili kukinga ugonjwa huo kwa muda mrefu. Dozi ya kwanza inapendekezwa kwa watoto wenye miezi 12 hadi miezi 18. Dozi ya pili kwa kawaida watoto wanapewa wakiwa wana miaka miwili hadi sita.[1] Kwa watoto ambao hawajachanjwa akiugua anaweza kupewa dozi kinga.[3]

Kinga ya matumbwitumwi ni salama na haina mathari yanayosumbua sana.[1][3] Unaweza kuwa na maumivi madogo na uvimbe sehemu iliyochanjwa na homa kidogo. Na sio kawaida kuwa na marathi mengineyo.[1] Hakuna ushahidi wa kutosha wa kusema chanjo inahusiana na matatizo mengine ya mishipa ya fahamu.[3] Chanjo haitakiwi ipewe kwa wakina mama wenye mimba au wale ambao wana matatizo sugu ya kudhoofisha mfumo wa kulinda mwili.[1] Matokeo sio mazuri kwa watoto ambao mama zao walichanjwa wakati wakiwa na mimba zao; isipokuwa, utafiti zaidi bado haujafanywa.[1][3] Ingawa chanjo hiyo inatengenezwa kwenye viseli vya kuku, inaweza kutumika kwa wale ambao wana uzio au aleji ya mayai.[3]

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Asilimia kubwa ya nchi zilizoendelea na katika nchi zinazoendelea huwa wanafanya chanjo hiyo iwepo kwenye mpango wa taifa wa kueneza chanjo ikiwa ni pamoja na chanjo zingine surua na chanjo ya rubella inayojulikana kama MMR.[1] Mchanganyiko wa chanjo hizo tatu za mwanzo pamoja na chanjo ya tetekuwanga hujulikana kama MMRV ambayo pia hupatikana.[3] Tangu mwaka 2005 nchi 110 zimetoa chanjo kwa njia hii. Kwenye maeneo ambayo chanjo hiyo inatumika sana imesababisha upungufu wa zaidi ya asilimia 90% ya ugonjwa. Kadri ya nusu bilioni ya dozi ya aina mmoja ya chanjo imeshatolewa.[1]

Historia, jamii na majaribio ya chanjo

[hariri | hariri chanzo]

Leseni ya chanjo ya surua ilitolewa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1948; ingawa ufanisi wake haukudumu sana.[3] Chanjo zilizoboreshwa zilianza kuuzwa mnamo mwaka 1960s. Ingawa chanjo za mwanzo zilikuwa Isiyo rasmi chanjo zilizofuatia ni virusi vilivyo hai visivyokuwa na nguvu.[1] Imeandikwa kwenye kitabu cha Orodha ya Madawa Muhimu ya Shirika la Afya Duniani, ni dawa muhimu zinazohitajika kwa ajili ya msingi wa afya.[4] Kuna aina nyingi ya chanjo zinazotumika tangu mwaka 2007.[1]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 "Mumps virus vaccines" (PDF). Weekly epidemiological record. 82 (7): 49–60. 16 Feb 2007. PMID 17304707.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Hviid A, Rubin S, Mühlemann K (Machi 2008). "Mumps". The Lancet. 371 (9616): 932–44. doi:10.1016/S0140-6736(08)60419-5. PMID 18342688.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 3.6 Atkinson, William (Mei 2012). Mumps Epidemiology and Prevention of Vaccine-Preventable Diseases (tol. la 12). Public Health Foundation. ku. Chapter 14. ISBN 9780983263135.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "WHO Model List of EssentialMedicines" (PDF). World Health Organization. Oktoba 2013. Iliwekwa mnamo 22 Aprili 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chanjo ya matumbwitumwi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.