Nenda kwa yaliyomo

Chanjo ya BCG

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chanjo ya BCG
Microscopic image of the Calmette-Guérin bacillus, Ziehl–Neelsen stain, magnification:1,000nn
Vaccine description
Target disease Tuberculosis
Type Live bacteria
Clinical data
AHFS/Drugs.com Kigezo:Drugs.com
Pregnancy cat. C(US)
Legal status -only (US)
Routes Percutaneous
Identifiers
ATC code J07AN01
DrugBank DB12768
ChemSpider none

Chanjo ya Bacillus Calmette–Guérin (BCG) ni chanjo ambayo kimsingi hutumika dhidi ya kifua kikuu.[1]

Katika nchi ambazo kifua kikuu ni kawaida, kipimo kimoja cha dawa kinapendekezwa kwa watoto walio na afya nzuri sawa na afya yao wakati wa kuzaliwa.[1] Watoto walio na virusi vya UKIMWI wanafaa kupewa chanjo.[2] Katika maeneo ambayo kifua kikuu si kawaida, watoto tu wenye hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo hupewa chanjo na sehemu zinazoshukiwa kupimwa na kutibiwa. Watu wazima ambao hawana ugonjwa wa kifua kikuu na hawakupewa chanjo lakini mara kwa mara miili yao hukataa kutumia dawa, kifua kikuu kinaweza pia kupewa chanjo.[1]

Viwango vya kinga hutofautiana sana na hudumu kwa kati ya miaka kumi na ishirini.[1] Miongoni mwa watoto, chanjo hii huzuia karibu 20% dhidi ya kupata ugonjwa na miongoni mwa wale ambao huathiriwa husaidia nusu yao dhidi ya kupata ugonjwa huo.[3] Chanjo hii hutolewa kwa kudungwa sindano mwilini.[1] Vipimo vya ziada haviungwi mkono kwa ushahidi.[1] Pia, inaweza kutumika katika matibabu ya baadhi ya aina nyingine ya saratani ya kibofu cha mkojo.[4]

Athari kuu ni nadra. Mara nyingi kuna wekundu, kuvimba, na uchungu mkali kwenye sehemu iliyodungwa sindano. Kidonda kidogo pia kinaweza kujiunda na kuacha kovu baada ya kupona. Madhara ni ya kawaida sana na yanaweza kuwa makali sana kwa wale ambao wana kinga duni. Si salama kwa matumizi wakati wa ujauzito. Chanjo hii iliasisiwa kutoka kwa Mycobacterium bovis ambayo hupatikana sana kwa ng'ombe. Huku ishafanywa kuwa hafifu bado ipo na inafanya kazi.[1]

Chanjo ya BCG ilitumika mara ya kwanza mwaka wa 1921.[1] Ipo kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika La Afya Duniani, dawa muhimu zaidi inayohitajika kwenye mfumo wa afya.[5] Bei ya jumla ni dola 0.16 kwa kila kipimo mnamo 2014. Gharama yake Marekani ni kati ya dola 100 na 200.[6] Kila mwaka chanjo hii hutolewa kwa watoto karibu milioni 100.[1]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 1.8 "BCG Vaccine: WHO position paper" (PDF). Weekly epidemiological record. 4 (79): 25-40. Jan 23, 2014.
  2. "Revised BCG vaccination guidelines for infants at risk for HIV infection" (PDF). Wkly Epidemiol Rec. 82 (21): 193-196. May 25, 2007. PMID 17526121.
  3. Roy, A; Eisenhut, M; Harris, RJ; Rodrigues, LC; Sridhar, S; Habermann, S; Snell, L; Mangtani, P; Adetifa, I; Lalvani, A; Abubakar, I (5 August 2014). "Effect of BCG vaccination against Mycobacterium tuberculosis infection in children: systematic review and meta-analysis". BMJ (Clinical research ed.). 349: g4643. PMID 25097193.
  4. Houghton, BB; Chalasani, V; Hayne, D; Grimison, P; Brown, CS; Patel, MI; Davis, ID; Stockler, MR (May 2013). "Intravesical chemotherapy plus bacille Calmette-Guérin in non-muscle invasive bladder cancer: a systematic review with meta-analysis". BJU International. 111 (6): 977–83. PMID 23253618.
  5. "WHO Model List of EssentialMedicines" (PDF). World Health Organization. October 2013. Retrieved 22 April 2014.
  6. Hamilton, Richart (2015). Tarascon Pocket Pharmacopoeia 2015 Deluxe Lab-Coat Edition. Jones & Bartlett Learning. p. 312. ISBN 9781284057560.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chanjo ya BCG kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.