Nenda kwa yaliyomo

Chancel Mbemba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chancel Mangulu Mbemba (alizaliwa 8 Agosti 1994), na ni mchezaji wa soka wa kitaalamu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, akiichezea klabu ya Ligue 1, Lille, na pia kuwa nahodha wa timu ya taifa ya DR Congo.

Mbemba alianza taaluma yake ya kitaalamu na Anderlecht, ambapo alishinda Belgian Pro League msimu wa 2013–14. Mwaka uliofuata, alihama Newcastle United, akicheza Premier League na kushinda EFL Championship mwaka 2017. Katika miaka minne aliyocheza Porto, alishinda double ya Primeira Liga na Taça de Portugal mnamo 2020 na 2022.

Kimataifa, Mbemba ameshiriki na timu ya taifa ya DR Congo tangu mwaka 2012, akiwa na zaidi ya michezo 90 na kuwakilisha nchi yake katika mashindano matano ya Africa Cup of Nations, akimaliza nafasi ya tatu mwaka 2015.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chancel Mbemba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.