Chama cha Kikomunisti cha Kampuchea

Chama cha Kikomunisti cha Kampuchea (kwa Kikambodia: Kanakpak Kommuynis Kampuchea) kilikuwa chama cha kisiasa cha msimamo mkali nchini Kamboja kilichoanzishwa mnamo mwaka 1960 na kuja kufahamika zaidi duniani kote kupitia mabaki ya jeshi lake la msituni yaliyopewa jina la Khmer Rouge. Chama hiki kiliongozwa na katibu mkuu wake Saloth Sar anayefahamika kama Pol Pot kuanzia mwaka 1963 hadi kiliposambaratika huku kikifuata misingi ya kiitikadi iliyochanganya Ukomunisti wa Mao Zedong na uzalendo uliopitiliza wa kikabila uliolenga kuunda jamii mpya inayotegemea kilimo pekee bila uwepo wa miji, fedha, elimu ya kisasa, wala athari zozote za kigeni.
Katika maisha yake yote chama kilitenda kazi zake kwa siri kubwa chini ya jina la "Angkar" ambalo linamaanisha "Shirika" ambapo hata wananchi wengi wa Kambodia hawakujua jina rasmi la chama hicho wala viongozi wake wakuu hadi miaka miwili baada ya wao kushika hatamu za nchi. Baada ya kuendesha vita vya msituni kwa miaka miangi chama kilifanikiwa kupindua serikali ya kijeshi ya Jamhuri ya Khmer mnamo tarehe 17 Aprili 1975 na kuanzisha serikali ya kidikteta ya Kampuchea ya Kidemokrasia iliyodumu hadi mwaka 1979. Ndani ya kipindi hiki kifupi cha utawala wake chama kilitekeleza sera za kinyama zilizosababisha vifo vya takriban watu milioni mbili kupitia mauaji ya makusudi ya wasomi na viongozi wa kidini, njaa ya kulazimishwa, na kufanyishwa kazi ngumu vijijini zilizopelekea nchi hiyo kukumbwa na janga kubwa la mauaji ya kimbari. Serikali ya chama hiki iliangushwa rasmi mnamo Januari 1979 kufuatia uvamizi wa kijeshi wa nchi jirani ya Vietnam ulioungwa mkono na waasi wa ndani ya nchi hiyo na kuwalazimisha viongozi wake kukimbilia tena milimani ambako mnamo Desemba 1981 kilitangaza rasmi kujivunja ili kupisha mikakati mipya ya kisiasa ingawa wanachama wake waliendelea kupigana kama kikundi cha waasi hadi mwishoni mwa miaka ya 1990 uongozi wao uliposambaratika kabisa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Chandler, David P. (1999). Voices from S-21: Terror and History in Pol Pot's Secret Prison. University of California Press.
- Short, Philip (2004). Pol Pot: Anatomy of a Nightmare. Henry Holt and Company.
| Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chama cha Kikomunisti cha Kampuchea kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |