Chakula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 17:34, 4 Novemba 2015 na Kipala (majadiliano | michango) (kiungo)
Vyakula vyenye asili ya mimea
Aina za nyama.

Chakula ni kile kinacholiwa na watu kwa kudumisha maisha yao. Mwili unahitaji virutubishi, nishati na maji. Haya yote hupatikana katika chakula.

Virutubishi vya mwili ni hasa yafuatayo:

Protini, mafuta na wanga huleta nishati ya mwili. Vilevile hukuza mwili yaani katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula (tumboni) zinapasuliwa kwa sehemu asilia zao na kuingizwa katika muundo wa seli za mwili.

Chakula kinatoka kwenye mimea na pia kwenye wanayama. Sehemu ya mahitaji yanatoka pia moja kwa moja kwenye mazingira bila kupita mimea au wanyama hasa madini kwa mfano chumvi.

Lakini chakula si pekee kazi ya kibiolojia na kifiziolojia kina upande wa kiutamaduni na kijamii vilevile.

Kila nchi ina chakula chake na watu wamezoea vyakula pamoja na namna ya kutayarisha vyakula vyao.

Chakula na afya

Chakula kinatakiwa kuwa na sehemu zote zinazohitajika na mwili. Uhaba wa sehemu mmoja utasababisha utapiamlo na magonjwa mbalimbali. Kuna matatizo hasa kama watoto hukosa chakula chenye ulinganifu. Mara nyingi wakinamama wanaowapa watoto chakula wanajali tu ya kwamba mtoto ashibe. Mtu anaweza kushiba kutokana na wanga pekee yake lakini uhaba wa protini na vitamini huleta utapiamlo na kusababisha magonjwa na ikitokea kwa watoto upungufu wa kukua kwa sehemu za ubongo na mwili.

Vilevilekuna tatizo la mara kwa mara ni uhaba wa minerali fulani katika mazingira ya pekee.

Chakula kinahusiana na afya pia kuhusu uwingi au uhaba wake. Inaeleweka ya kwamba uhaba wa chakula yaani njaa kwa muda mrefu unadhoofisha mwili na afya. Lakini kinyume chake kuzidi kwa chakula kinaleta hatari pia. Katika maisha ya mjini na familia waliotoka katika umaskini kali hali ya kunona tangu utotoni imekuwa tatizo kubwa. Kunona kunafupisha maisha na kuandaa mwili kwa magonjwa mengi yasiyotokea kwa uzito wa wastani mwilini.


Vyakula vya kibinadamu
Asili ya mimea Asili ya wanyama


Viungo vya Nje