Celeste Ntuli

Celeste Ntuli (alizaliwa Agosti 25, 1979) ni mchekeshaji na mwigizaji kutoka Afrika Kusini. Anajulikana sana kama malkia wa vichekesho vya Kizulu, na anajulikana kwa kuwa mchekeshaji wa kwanza wa kike wa nchini humo kurekodi DVD ya onyesho la mtu mmoja.
Miaka ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Ntuli alizaliwa Empangeni ambako alipata elimu yake ya msingi na sekondari. Yeye ni mtoto wa sita kati ya watoto wanane. Familia yake ilihamia Durban, ambako alisomea teknolojia ya burudani katika Durban University of Technology.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2005, alifanya onyesho lake la kwanza la ucheshi katika kanisa moja huko Durban. Mwaka 2009, alikuwa mmoja wa waliofika hatua ya mwisho katika msimu wa pili wa mashindano ya So You Think You're Funny ya SABC 1. Alianza kazi yake ya kitaalamu katika ucheshi mwaka 2010. Kwa sasa anajulikana kwa kuwa mchekeshaji wa kwanza kurekodi DVD ya onyesho la mtu mmoja lililoitwa Seriously, Celeste.
Filamu alizoshiriki
[hariri | hariri chanzo]Ameshazishiriki katika filamu na vipindi kadhaa, vikiwemo:
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://briefly.co.za/35748-celeste-ntuli-biography.html
- ↑ https://www.tvsa.co.za/actors/viewactor.aspx?actorid=15414
- ↑ https://whacked.co.za/celeste-ntuli/
| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Celeste Ntuli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |