Nenda kwa yaliyomo

Caroline LeCount

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Caroline Rebecca Le Count (takriban 1846 – 24 Januari 1923; mara nyingi huandikwa LeCount) alikuwa mwalimu na mwanaharakati wa haki za kiraia kutoka Philadelphia, Pennsylvania, nchini Marekani. Mara nyingi hulinganishwa na mwanaharakati wa baadaye Rosa Parks kutokana na juhudi zake za awali za kupinga ubaguzi katika usafiri wa umma.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Le Count alizaliwa South Philadelphia mwaka 1846 akiwa mmoja wa watoto wanne. Baba yake, James LeCount, alikuwa fundi wa kutengeneza makabati na pia mtoa huduma za mazishi. Inaaminika kuwa alihusika katika Underground Railroad, kwa kuwa simulizi za kifamilia zinaeleza kuwa alikuwa akiwaficha watumwa waliotoroka ndani ya majeneza.[1][2][3]

Caroline alianza masomo akiwa mdogo na alihitimu akiwa mwanafunzi bora katika darasa lake la wanafunzi watano kutoka Institute for Colored Youth mwaka 1863.[4][5]

  1. ↑ [(http://inherownright.org/spotlight/biographical-profiles/feature/caroline-lecount-the-ohio-street-school) "Caroline LeCount & the Ohio Street School"]. Biographical Profiles - Explore the story of women's activism through documents & images (kwa Kiingereza). 3 Oktoba 2020. Iliwekwa mnamo 24 Septemba 2022. {{cite web}}: Check |url= value (help)[dead link]
  2. ↑ Lane, 1991, uk. 126.
  3. ↑ Biddle, 2010, uk. 118.
  4. ↑ [(https://catto.ushistory.org/catto_people/caroline-lecount/) "Caroline LeCount"]. catto.ushistory.org. Iliwekwa mnamo 24 Septemba 2022. {{cite web}}: Check |url= value (help)[dead link]
  5. ↑ Biddle, 2010, uk. 288.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Caroline LeCount kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.