Carlo Acutis

Carlo Acutis (3 Mei 1991 – 12 Oktoba 2006) alikuwa kijana mzaliwa wa Uingereza [1] mbunifu wa tovuti wa Kiitalia ambamo aliandika miujiza kuhusiana na Ekaristi takatifu na kuhusu matokeo ya Bikira Maria duniani yaliyoidhinishwa, na kuyapanga mambo hayo yote kwenye tovuti aliyoibuni kabla ya kifo chake kilichotokana na saratani ya damu.
Acutis alijulikana kwa uchangamfu wake, ustadi wa kutumia kompyuta, na kujitolea kwa ajili ya kuandika na kutunza masuala yahusuyo Ekaristi takatifu, ambayo ilikuwa mada kuu ya maisha yake.
Alitangazwa mwenye heri na Papa Fransisko tarehe 10 Oktoba 2020. Baada ya muujiza wa pili unaohusishwa na maombezi ya Acutis kuthibitishwa mnamo Mei 2024, Papa huyo alitoa kibali mnamo Julai 2024 ili atangazwe mtakatifu tarehe 27 Aprili 2025. [2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Syed, Armani (2024-05-24). "British-Born Teenager Set to Become First Millennial Saint". TIME (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-11-04.
- ↑ Mares, Courtney (20 Nov 2024). "Pope Francis announces 2025 canonizations for Carlo Acutis, Pier Giorgio Frassati during Jubilee celebrations". Catholic News Agency.
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |