Nenda kwa yaliyomo

Carl Hilty

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Carl Andreas Hilty (28 Februari 183312 Oktoba 1909) alikuwa wakili, profesa wa sheria na katiba, mwanasiasa, mwanafalsafa, mwanateolojia na mwandishi kutoka Uswisi.

Alizaliwa katika mji mdogo wa Werdenberg, ulioko St. Gallen, kaskazini-mashariki mwa Uswisi. Baba yake, daktari Johann Ulrich Hilty, alikuwa akifanya kazi ya udaktari mjini Chur, mji mkuu wa Grisons mashariki. Familia ya Hilty iliishi Werdenberg kwa karne nyingi, na mnamo mwaka 1835 walinunua Kasri la Werdenberg katika mnada.[1][2][3]

Carl Hilty alikulia Chur na kusoma shule za umma na shule ya kanisa. Alisoma sheria Ujerumani na kupata udaktari wa sheria Heidelberg 1854. Alitumia muda mwingi London na Paris ili kujiboresha katika lugha. Kutoka 1855, Alimiliki na kuongoza kampuni yake ya sheria mjini Chur na kupigania demokrasia ya moja kwa moja. Alimuoa Johanna Gaertner 1857. Hilty alikuwa profesa wa sheria ya katiba Bern 1874, msemaji wa haki za wanawake, na mwanaharakati wa usawa. Aliandika juu ya furaha, maana ya maisha, na maadili, kazi zake zikajulikana kimataifa.

  1. "Die Familie Hilty in Städtli und Schloss". schloss-werdenberg.ch (kwa Kijerumani). 2014. Iliwekwa mnamo 2021-03-01.
  2. Mattmüller, Hanspeter. "Hilty, Carl". Deutsche Biographie (kwa Kijerumani). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Julai 2021. Iliwekwa mnamo 26 Februari 2021.{{cite encyclopedia}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Petrig Schuler, Eva (2010-01-13). "Hilty, Carl". Historisches Lexikon der Schweiz (HLS) (kwa Kijerumani). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-05. Iliwekwa mnamo 2021-03-01.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carl Hilty kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.