Nenda kwa yaliyomo

Carine Goren

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Carine Goren ( alizaliwa mwaka 1974) ni Mpishi wa vitindamlo (pastry chef) kutoka Israeli, mwandishi wa vitabu vya mapishi vilivyouza sana, na mtu wa televisheni.

Alianza kazi yake ya upishi akiwa na umri wa miaka 26 kama mwandishi na mhariri wa mapishi katika jarida la chakula la Israel liitwalo Al Hashulchan (yaani “Kwenye Meza”). Mwaka 2006 alichapisha kitabu chake cha kwanza cha mapishi ya vitamu kiitwacho Sweet Secrets. Kufikia mwaka 2016 alikuwa amechapisha jumla ya vitabu vitano vya mapishi, likiwemo moja la watoto.

Pia ana kipindi chake cha televisheni cha upishi cha kuoka keki kinachoitwa Sweet Secrets. Mwaka 2016 alikua jaji katika kipindi kipya cha uhalisia cha Israel kiitwacho Bake-Off Israel. Alikuwa mtu aliyesomewa zaidi kwenye Google nchini Israel mwaka 2015.[1]

  1. McCluskey, Megan (30 Desemba 2015). ["See) the Most Googled Person in Each Country in 2015". Time. Iliwekwa mnamo 22 Novemba 2016. {{cite web}}: Check |url= value (help)[dead link]
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carine Goren kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.