Nenda kwa yaliyomo

Camille Vidart

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Camille Vidart (18541930) alikuwa mchambuzi wa elimu, mtafsiri, mpigania haki za wanawake, na mpenda amani kutoka Uswisi. Alijihusisha sana na mashirika ya wanawake, ikiwemo Shirikisho la Kimataifa la Abolitionist na Chama cha Kimataifa cha Wanawake kwa Amani na Uhuru.

Vidart pia alitafsiri kitabu maarufu cha Heidi kutoka Kijerumani hadi Kifaransa na alijitahidi kupigania haki ya wanawake kushiriki katika uchaguzi nchini Uswisi, ingawa hakupata mafanikio makubwa.[1][2][3]

Vidart, c. 1890

Baada ya kuhitimu, Camille Vidart alianza kufundisha katika shule ya wasichana ya École Peschier mjini Geneva mwaka 1874. Mnamo 1879, aliweza kujiunga na shule ya upili ya wasichana (Höhere Töchterschule) huko Zürich, akitajwa kama mwanamke wa kwanza kufundisha huko. Alifundisha hadi 1884 na alifahamiana na Johanna Spyri(mwandishi wa kitabu cha Heidi), kisha akatafsiri kitabu cha Heidi kwa Kifaransa. Baada ya hapo alihamia Lausanne (18841886)

Mnamo miaka ya 1890, Vidart alianza kujitolea kwenye mashirika kadhaa ya wanawake ndipo akanzisha shirikisho la wanawake la Uswisi na kuunga mkono haki za kupiga kura. Baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia, alikua msomi wa amani na mwanachama wa Women's International League for Peace and Freedom.

Camille Vidart alifariki mjini Geneva tarehe 29 Juni 1930.[4][5]

  1. "Camulle Vidart" (kwa Kifaransa). Dictionnnaire Historique de la Suisse. 30 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 20 Januari 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Piguet, Laure. "Camille Vidart" (kwa Kifaransa). 100 Elles. Iliwekwa mnamo 20 Januari 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Mlle Camille Vidart" (kwa Kifaransa). Le Mouvement Féministe. 12 Julai 1930. Iliwekwa mnamo 20 Januari 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Clara Guthrie d'Arcis" (kwa Kifaransa). Dictionnaire Historique de la Suisse. 16 Machi 2006. Iliwekwa mnamo 21 Januari 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "World Union of Women for International Concord". Lonsea. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-05-17. Iliwekwa mnamo 21 Januari 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Camille Vidart kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.