Camille Drevet
Camille Drevet née Bonnat (21 Juni 1881 – 18 Mei 1969) alikuwa Mfaransa aliyepinga ukoloni, mwanaharakati wa wanawake, na mpigania amani. Alishirikiana sana na tawi la Ufaransa la Ligi dhidi ya Ubeberu na aliwahi kuwa katibu wa kimataifa wa Ligi ya Wanawake kwa Amani na Uhuru. (LIFPL).[1][2]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tarehe 29 Agosti mwaka 1904, Drevet aliolewa na Henri-Paul Drevet, ambaye alifariki kwenye Vita ya Kwanza ya Dunia. Drevet alihusika sana katika haki za wanawake na kupinga vita, alianzisha kundi la "La Ligue d'action féminine pour le suffrage des femmes" (kundi la wanawake lililoundwa Ufaransa mnamo mwaka 1925 linalolenga kupigania sauti ya wanawake) na kuwa mhariri wa gazeti la "La Voix des femmes". Alihudhuria mikutano ya kimataifa ya WILPF na safari za Ulaya na Asia, akitekeleza kazi za amani. Mnamo mwaka1930, aliteuliwa kuwa katibu wa kimataifa wa WILPF, pia akihudumu kama katibu wa Les Amis de Gandhi, (shirika lililoundwa kueneza mafundisho na ujumbe wa Mahatma Gandhi kuhusu amani, upendo, na kutokutoa vurugu akieneza ujumbe wa amani na haki. [3]
Kifo
[hariri | hariri chanzo]Camille Drevet alifariki Annecy, Mei 18, 1969.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Dreyfus, Michel (16 Oktoba 2021). "DREVET Camille, Eugénie (née BONNAT)". maitron.fr (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 13 Januari 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Boittin, Jennifer Anne (27 Oktoba 2022). Undesirable: Passionate Mobility and Women's Defiance of French Colonial Policing, 1919–1952. University of Chicago Press. uk. 94. ISBN 978-0-226-82225-9. OCLC 1300752477.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Keryell, Jacques, mhr. (1 Januari 1997). Louis Massignon et ses contemporains. KARTHALA Editions. uk. 153. ISBN 978-2-86537-736-7. OCLC 1025914447.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Camille Drevet kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |