Nenda kwa yaliyomo

Calvin Ramsay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Calvin William Ramsay (amezaliwa 31 Julai 2003) ni mchezaji wa soka wa Kiskoti ambaye kwa sasa anacheza kama beki wa kulia wa klabu ya Ligi Kuu Uingereza Liverpool F.C. na timu ya taifa ya Uskoti.

Maisha katia klabu

[hariri | hariri chanzo]

Aberdeen

[hariri | hariri chanzo]

Calvin katika safu ya vijana huko Aberdeen, alicheza mechi yake ya kwanza kwa kuingizwa kama mchezaji wa akiba dhidi ya timu ya Dundee United mnamo machi 2021, chini ya meneja wa muda Paul Sheerin. Ramsay aliendelea kucheza mechi nyingine tano katika msimu wake wa kwanza akiwa na timu ya wakubwa, Aberdeen FC. Mnamo tarehe 27 Agosti 2021 alicheza mechi yake ya kwanza ya Uropa katika klabu hiyo dhidi ya BK Häcken ya Uswidi Julai 2021 katika mechi ya kufuzu Ligi ya UEFA conference. Alianza nyuma kama beki wa kulia na ushindi wa 5-1 na kusaidia bao la kwanza la mchezo. Ramsay alishinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa SFWA kwa 2021–22, msimu wake pekee kamili akiwa na Aberdeen.

Liverpool

[hariri | hariri chanzo]

Ramsay alihamia klabu ya Liverpool ya Ligi Kuu ya Uingereza Juni 2022. Alitia saini mkataba wa miaka mitano kwa ada ya awali ya £4.2m,[1] mauzo makubwa katika rekodi ya klabu ya Aberdeen.[2]

  1. Sanghera, Mandeep (19 Juni 2022). "Calvin Ramsay: Liverpool sign Aberdeen right-back for £4.2m". BBC Sport. Iliwekwa mnamo 19 Juni 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Marini, Gianni (19 Juni 2022). "Calvin Ramsay departs Aberdeen for Liverpool in club-record deal". STV News. Iliwekwa mnamo 19 Juni 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Calvin Ramsay kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.