Calixthe Beyala
Calixthe Beyala (alizaliwa Sa'a, Kameruni, 1961) ni mwandishi wa Kameruni - Ufaransa anayeelezea kazi zake kwa lugha ya Kifaransa.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Mwanachama wa kabila la Beti, Calixthe Beyala alizaliwa na wazazi wa Kameruni.
Shangazi yake na bibi yake walikuwa na ushawishi mkubwa katika ukuaji wake, na alikuwa akisikiliza hadithi za bibi yake, hadithi ambazo zilimpa motisha ya kufanya kazi kwa bidii na kujenga taaluma yenye maana.[1]
Beyala alisoma shule ya École Principale du Camp Mboppi huko Douala na baadae shule ya Lycée des Rapides huko Bangui na Lycée Polyvalent de Douala. Mwisho alishinda ufadhili wa masomo kwenda Paris akiwa na umri wa miaka kumi na saba, ambapo kutokana na utendaji mzuri wa kitaaluma alipata Baccalaureate. [2] [3]
Baada ya kuishi kwa miaka kadhaa nchini Hispania, alichapisha kitabu chake cha kwanza kilichofahamika kwa jina la C'est le soleil qui m'a brûlée, akiwa na umri wa miaka 23, na baadae akaamua kuwa mwandishi wa kujitegemea wa muda wote.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Jagne, Siga Fatima; Parekh, Pushpa Naidu (2012). Postcolonial African Writers: A Bio-bibliographical Critical Sourcebook. Routledge. ku. 75–82. ISBN 978-1-136-59397-0.
- ↑ "Calixthe Beyala", The Literary Encyclopedia
- 1 2 "Calixthe Beyala : writing in the margins", Africultures, Boniface Mongo-Mboussa
| Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Calixthe Beyala kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |