Cécile Manorohanta
Cécile Manorohanta (jina kamili: Cécile Marie Ange Manorohanta) ni mwanasiasa kutoka Madagaska ambaye amehudumu katika serikali ya nchi hiyo kama naibu waziri mkuu anayeshughulikia mambo ya ndani tangu mwaka 2009. Hapo awali alikuwa Waziri wa Ulinzi kuanzia 2007 hadi 2009.
Manorohanta aliteuliwa kuwa waziri wa ulinzi mnamo 27 Oktoba 2007 katika serikali ya Waziri Mkuu Charles Rabemananjara. Alikuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa waziri wa ulinzi nchini kwake.[1]
Mnamo 9 Februari 2009, Manorohanta alitangaza kujiuzulu, akisema kwamba "baada ya yote yaliyotokea, nimeamua kuanzia sasa kutoendelea kuwa sehemu ya serikali hii,"[2] akimaanisha tukio la mauaji ya tarehe 7 Februari, wakati wa Maandamano ya Madagaska ya 2009, ambapo polisi waliwapiga risasi na kuwaua waandamanaji 50.[3] Mkuu wa majeshi Mamy Ranaivoniarivo aliteuliwa kuchukua nafasi ya Manorohanta siku hiyohiyo.[4][5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Madagascan leader names new government" Archived 2009-02-15 at the Wayback Machine The Times, 27 October 2007
- ↑ Madagascar defense minister resigns
- ↑ "Madagascar protesters shot dead". Al Jazeera. 2009-02-08. Iliwekwa mnamo 2009-02-08.
- ↑ "Defence minister quits over Madagascar bloodbath", AFP, 9 February 2009.
- ↑ "SADC 'rejects, condemns' new Madagascar govt", AFP, 8 September 2009.
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Cécile Manorohanta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |