Nenda kwa yaliyomo

Bwawa la Weija

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bwawa la Weija ni bwawa lililojengwa kwenye Mto Densu nchini Ghana, ambalo linatumika kutoa maji katika kituo kikuu cha kutibu maji kwa ajili ya Jiji la Accra. Bwawa hili linaendeshwa na mamlaka ya maji ya Ghana.[1][2]

Bwawa la Weija linauwezo wa kutoa maji takribani asilimia 80 ya maji safi kwa matumizi kwa wakazi wa Accra na maeneo ya jirani. Ujenzi wake ulianza mwaka 1974 na kukamilika mwaka 1978 na kampuni ya Kiitaliano iliyojulikana kama Messrs Tahi.

Kumwagwa kwa maji ya bwawa

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Juni 2014, maji yalifunguliwa kutoka bwawani na kusababisha mafuriko katika eneo la Glefe. Baadhi ya waathirika walidai kuwa mafuriko hayo yalichangiwa na kutofanyika kwa uchimbaji wa mkondo wa mto unaoelekea baharini kutokana na kusubiri kumalizika kwa tamasha la Homowo.

Mwezi Machi 2017, Ghana Water Company ilianza kumwaga maji kutoka bwawani ili kuzuia kiwango cha maji kisizidi kiwango cha juu kinachoruhusiwa. Hatua hiyo ilihitajika kutokana na msimu wa mvua na ilisababisha mafuriko katika maeneo ya Tetegu na Oblogo.

Mwezi Machi 2021, malango ya bwawa yalifunguliwa baada ya kiwango cha maji kuongezeka ghafla kwa futi 1.9 ndani ya saa 24. Kiwango cha maji kiliongezeka kutoka futi 46.2 hadi futi 48.1, ambacho kilikuwa futi 1.1 juu ya kiwango salama cha uendeshaji cha futi 47. Kufunguliwa kwa malango kulifanyika ili kupunguza hatari ya bwawa kuharibika au kupasuka.

Mwezi Oktoba 2022, bwawa lilimwaga maji mara mbili kutokana na mvua kubwa. Kiwango cha maji kilikuwa futi 49.5 wakati wa kumwagwa kwa kwanza mwanzoni mwa mwezi huo, na futi 47.9 wakati wa kumwagwa kwa pili baadaye mwezi huo.

Bwawa la Weija ni mojawapo ya miundombinu muhimu zaidi ya maji nchini Ghana kutokana na mchango wake mkubwa katika usambazaji wa maji kwa mji mkuu wa Accra na maeneo yanayouzunguka.[3]

  1. Amoani Emmanuel Ofori. "NADMO - Weija Dam Spillage Ongoing ... Nadmo Success Story". www.nadmo.gov.gh (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-05-25. Iliwekwa mnamo 2026-06-23.
  2. "Spillage of Weija dam causes 'severe' flooding at Glefe, Opetekwei - MyJoyOnline.com". www.myjoyonline.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-21. Iliwekwa mnamo 2026-06-23.
  3. "Weija dam spillage causes flooding downstream". Graphic Online (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2022-10-04. Iliwekwa mnamo 2026-06-23.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ghana bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bwawa la Weija kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.